PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: PICHA 23 ZA MGOMBEA URAIS KWA TIKET YA CCM DR MAGUFULI JIJINI ARUSHA JANA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwasalimia ...





Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa sambamba na Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwasalimia wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha




Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa sambamba na Katibu 
Mkuu
wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwasalimia wakazi wa jiji la Arusha 
na vitongoji vyake kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni uliofanyika 
katika uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.



Mgombea Ubunge wa jimbo la Simanjiro na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za CCM,Ndugu Ole Sendeka akiwahutubia maelfu a wananchi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.



Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.



Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. 



Umati wa Wakazi wa jiji la Arusha na Vitongoji vyake wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Pombe Magufuli jijini humo.



Wananchi wa Arusha waliofurika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid wakionesha kufurahia Sera za Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.



Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa jimbo la Arusha mjini,Ndugu Phillemon Mollel mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha kwenye mkutano wa kampeni



Wakazi wa maeneo ya Jirani na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid waliacha Shughuli zao na Kufuatilia sera za Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.



Baadhi ya Wanachama wa Chadema wakirejesha kadi zao kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha



Wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya wakitumbuiza katika Mkutano huo wa kampeni.



Hapa ni kazi na dawa.......



Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi 
CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la 
Monduli,Namelok Moringe Sokoine kwenye mkutano wa kampeni ulofanyka 
mjini Monduli mapema leo mchana.



Mgombea
Ubunge jimbo la Monduli,Namelok Moringe Sokoine akitabasamu mara baada 
kunadiwa na Mgombea Urais wa CCM Dkt Maguli mbele ya wakazi wa mji wa 
Monduli (hawapo pichani) mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni 



Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli (wa pili kushoto),akiwa ameambatana na 
baadhi ya wajumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni ya CCM,wakishiriki 
sala ya pamoja ya kumuombea Marehemu,Waziri Mkuu wa zamani,Hayati Edward
Sokoine Moringe kwenye kabuli lake,Monduli juu,mkoani Arusha.



Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiweka shada la Maua kwenye kabuli la Waziri Mkuu wa zamani,Hayati Edward
Sokoine Moringe,ambapo pia akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni ya CCM,walishiriki 
sala ya pamoja ya kumuombea Marehemu,



Mke wa Marehemu Sokoine akisaidiwa kuweka shada la maua



Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi 
CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mtoto wa 
Marehemu,Hayati Edward Moringe Sokoine wakitoka nje ya Kabuli la Hayati 
Sokine mara baada ya kushiriki sala ya pamoja,Monduli juu mkoani Arusha.



Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa 
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni 
mjini Longido,mkoani Arusha




Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wakazi wa mji wa Longido,mara baada ya kuwahutubia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top