NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu ya
Riadha ya Mkoa wa Arusha imeanza imeanza kuweke mikakati ya kwenda katika
mashindano ya Rock City Marathoni yanayotarajia kufanyika mwezi ujao Mkoani
Mwanza.
Akizungumzia hilo Kocha wa Riadha Mkoani Arusha, Thomas John alisema kuwa, ili
kuhakikisha watakwenda kuchukua ubingwa tayari wameandaa mashindano ya ndani,
ili kuchagua wanariadha watakao kwenda kuwakilisha mkoa katika mashindano hayo.
“Ili
mwanariadha apate nafasi ya kuchaguliwa katika timu ya Mkoa lazima ashiriki
mashindano manne mfululizo na kufanikiwa kuingia katika kila hatua inayofuatwa”
alisema John.
Mashindano ya
Rock City Marathoni yanatarajia kufanyika Mkoani mwanza Septemba 15 mwaka huu,
yakishirikisha wanariadha kutoka ndani na nje ya Tanzania.
“Mkoa wetu
tunatarajia kupeleka zaidi ya wanariadha 30 Mkoani Mwanza, Kutokana na kupewa
nafasi kubwa ya wanaridha, Pia Mkoa wetu ulifanya vizuri katika mashindano ya
Rotary yaliyofanyika mwezi huu jijini Dar es Salaam yakiwa maalum ya kumuenzi
Baba wa Taifa Hayati Julias K. Nyerere” alisema John.
Hata hivyo
Kocha huyo alisema kuwa licha ya kujiandaa na mashindano hayo, tayari wameanza
mikakati ya kujiandaa na mashindano ya Nyika ya Cross Country yatakayofanyika
mwakani mwezi wa tatu katika nchi ya Uganda jijini Kampala.
Mashindano ya
Nyika yatafanyika katika makundi mawili
ambapo kundi la kwanza watashiriki mbio za Km 8, wakati kundi lingine
litashiriki Mbio za Km 12.
Post a Comment