PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UKATA NDIO CHANZO CHA MICHEZO KUSHUKA NCHINI.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. 0762 801099 Mara nyingi sana watanzania tumekuwa tukilalamika juu ya mwenendo mbaya kwa timu ...




NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA. 0762 801099

Mara nyingi sana watanzania tumekuwa tukilalamika juu ya mwenendo mbaya kwa timu zetu za michezo kuwa hazifanyi vizuri katika kila mashindano tunayoshiriki, tafauti na niaka ya nyuma ambapo nchi yetu ilikuwa na sifa kubwa katika riadha.

Miezi michache iliyopita nimegundua sababu moja ambayo inajitokeza kila idara ya michezo "UKATA", ndio tatizo kila kiongozi analia na tatizo hilo. Kwa kuthibitisha hilo angalia mifano michache mbele ya makala hii na utakubaliana nami.

Mapema mwezi huu mkurugezi wa Olimpiki Maalumu Frank Macha akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa kunahatihati timu ya riadha ya walemavu kushiriki mashindano ya dunia nchini Marekani kutokana na timu hiyo kushindwa kuingia kambini kutokana na kusekana kwa fedha za kuwaweka kambini ,pia kuwasafirisha wanamichezo hao.

Mfano wa pili pale uongozi wa chama cha mpira wa magongo taifa (THA) Nao kutembeza bakuli kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya mchezo huo kwenda Nchini Misri mwezi wa kumi katika mashindano ya kufuzu Olimpiki yanayotarajia kufanykia kuanzia Oktoba 16 hadi 27 mwaka huu.

Sio hilo tu ukibaki katika mchezo wa riadha tumekuwa tukishuhudia mara nyingi wanariadha wakikimbia peku peku kwa madai kuwa wameshindwa kupata fedha za kununulia vifaa.

Ikumbukwe kwamba mwanariadha toka Tanzania Daniel Thomas mwaka 1964 kwenye mashindano ya Olimpiki nchini Japan alizuiliwa kukimbia peku peku.

Nalo shirika la ngumi za ridhaa Tanzania (BFT) litangaza kuwalinahitaji zaidi ya sh milioni 100, ili kuiwezesha imu ya taifa ya mchezo huo kwenda kushiriki michuano ya vijana ya Afrka itakayofanyika mwezi ujao kuanzia tar 15 hadi 23 mjini Casablanca nchini Morocco

Haipendezi kuona nchi inapewa mwalikoa katika mashindano halafu taifa linakiri umasikini hata kuhakikisha wanaukata wa kushindwa kuipeleka Tanzania kushiriki kwenye michuano mbalimbali

Tujue kwamba katika michuano tunayoalikwa ndimo tunapokuja kujua uwezo wetu katika mchezo hali halisi ya wanamichezo wetu, na pia tunapata picha halisi ya wapi tulipo na tufanye nini ili tusonge mbele.

Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu manaridha Fabiani Joseph aliweza kutoa yaliyo moyoni mwake juu ya idara ya michezo ilivyo hapa nchini

“taifa linatia aibu sana kwani hata bajeti ya michezo haina mantiki kwasababu haikidhi wala haifatiliwi, taifa lenye uchungu katika idara ya mivhezo halina haya katika kutumia fedha zake kwa manufaa ya nchi”

“mawaridha anakwaa kwake (geto) halafu asubuhi anaamkia mazoezini bila kocha kujua mchezaji wake amekula nini, amelala wapi na ana hali gani hii ni hatari sana” alisema Joseph

Aliongeza kuwa hata katika kaiba iliyo pendekezwa hakuona michezo ikipewa kipau mbele walkati riadhaa pekee hndi iliyoiletea nchi yetu sifa miaka ya nyuma

hata ukiangalia suala la filamu nako bado tatizo linawaumiza vichwa, mara nyingi tumeshuhudia migongano kati ya mmiliki na msambazaji,kila mmoja akimtuhumu mwezake kunufaika zaidi.

Shauku yangu kuona siku moja Tanzania inakua moja ya nchi tishio katka suala la michezo na mataifa ya jirani waje kujifunza kwetu kama ilivyo kuwa katika riadha miaka ya nyuma.

Tusipende kulaumu kwa kujikwaa kasha kuanguka bali tunahitaji kuangalia ni wapi tulipojikwaa na hatimaye kujifuta vumbi na kusonga mbele kwa ujasili mkubwa.

Suala la ukata sio katika michezo tu bali kila idara inatatizo hilo, hivyo viongozi waache kisingizio cha ukata na hatimaye kushindwa kupeleka timu sehemu husika.

Hakuna michuano ambayo inakuja ghafla kwani yote inakuwa kwenye kalenda zetu, ajabu ni kipi hadi msingizie ukosefu wa fedha hamjui mnaleta sifa mbaya kwa taifa.

Mabaya zaidi wengi wenu mlikuwa wanamichezo na mnafahamu kila jambo lililopo katika idara hii, kwanini muweke wachezajin kambini na hatimaye kuvunja kambi kwa kisingizio hicho ili hali mlifahamu?

Ushirikiano, umoja na uzalendo ndivyo vitakavyotutoa hapa tulipo, juhudi binafsi zinahitajika kwa kila mtu kuanzia kwako ili kuinua michezo hapa nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top