NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Chama
cha ngumi za ridhaa mkoani hapa (AABA),kinategemea kufanya mkutano mkuu
muda wowote kuanzia sasa ili kuweka mikakati ya chama hicho kwa miaka
mitano ya baadae.
Akizungumza
na gazeti hili katibu mkuu wa AABA Mohamed Abubakari, alisema kuwa wapo
katika hatua za mwisho kukutana na wadau mbali mbali wa ngumi wa kutoka
mkoani hapa na wengine nje ya Arusha ili kukiimalisha chama kwa faida
ya vizazi vijavyo.
“tunahitaji
kuweka mipango kazi ya miaka mitano ijayo kuanzia sasa, ili
kukiimalisha zaidi chama, na kuongeza nguvu kazi hasa kwa vijana ambao
wataitangaza Arusha kwa siku za mbele” alisema Abubakari.
Aliongeza
kuwa baada ya mkutano huo AABA hakitashiriki mashindano yoyote nje ya
mkoa wa Arusha kwa miaka miwili mfululizo ili kuwapima na kuwaivisha
vijana wao.
“wachezaji
watakao toka kushiriki mashindano nje ya Mkoa waetu ni wale waliokuwa
kwenye timu ya taifa pekee, hawa wengine hatutawaruhusu hadi watakapo
kuwa wameiva vizuri katika miaka hiyo miaka miwili” aliongeza kusema
Abubakari.
Aliongeza
kuwa ndani ya miaka miwili AABA watakuwa wameanzisha kliniki mbalimbali
za mchezo wa ngumi pamoja na kufanya matamasha mengi ili kuwahamasisha
watoto wadogo.
Katibu
huyo alitoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kuwaruhusu vijana wao
kushiriki mchezo huo akisema kuwa ni mchezo wenye faida kubwa ikiwa
pamoja na ajira na ulinzi wa afya zao.
Post a Comment