KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameongoza timu ya chama hicho kumsafishia njia Mgombea Urais wao, Dk John Magufuli mkoani Kilimanjaro, huku akiwaambia wananchi wa mkoa huo kuwa mgombea huyo ndiye kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania.
Akizindua
kampeni za CCM mjini Moshi, Kinana aliongozana na mgombea ubunge wa
Jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher ole Sendeka na yule wa
Mtera mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaj.
Kinana
alimuelezea Magufuli kuwa ni kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania
kutokana na historia yake ya uadilifu na uchapakazi katika maisha yake
yote ya utendaji serikalini.
Alisema katika utendaji wake akiwa Waziri kwa miaka 20, amefanya kazi kubwa kwa uadilifu na kujituma.
Akimuelezea
zaidi Magufuli, Kinana alisema mgombea huyo ameahidi Baraza dogo la
Mawaziri, hajatumia fedha kupata nafasi ya kugombea urais wala hana
makundi.
“Hana makundi...wapo waliochangisha fedha wamekusanya watu baadaye wanakuja kuwa mzigo.
"Yeye
Hana makundi wala hana mzigo. Hajaenda wilayani ama mikoani bali
alienda matawini,” alieleza Kinana ambaye pia alimuombea kura mgombea
ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha.
Kwa
upande wake, Ole Sendeka alisema ni lazima Watanzania wawapime wagombea
kwa kujua ukweli, si kwa kudanganyana na kuepuka dhambi ya ubaguzi wa
aina yoyote.
Post a Comment