Akizungumza kwa niaba ya UKAWA,Mwenyekiti Wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia alisema kuwa taarifa ya taasisi hiyo imeidhalilisha TWAWEZA wenyewe na CCM kwa ujumla.
"TWAWEZA imejidhalilisha kwa kubagua wagombea urais Wa vyama vingine mbali na CCM na CHADEMA"
"TWAWEZA haifahamu hata idadi ya wagombea ubunge na udiwani,utafiti huo umetoa ripoti inayokinzana na ukurasa Wa saba,huu utafiti ni Wa uongo" alisema Mbatia.
"Katika taarifa ya TWAWEZA haijaweza kuhakiki taarifa yake kitakwimu,CCM imekubaliana na idadi ya watu walioshiriki kwenye utafiti kwa kigezo cha idadi ya watu 1848"
"CCM hiyo hiyo ilikataa kukubali maoni ya wananchi zaidi ya laki tatu kwenye rasimu ya katiba ya Warioba,lakini leo wamekubali watu 1848" aliongeza Mbatia.
"Simu za mkononi na chaja zilizogawiwa ilikuwa ni rushwa iliyotolewa na TWAWEZA kwa washiriki Wa utafiti huo"
"TWAWEZA wanajua vyama vya CUF,NCCR-MAGEUZI,na NLD hawajatoa wagombea wao Wa urais isipokuwa CHADEMA ila wameweka swali hilo,kwakuwa TWAWEZA ni taasis inayothamini midahalo tunawaalika kwenye midahalo ya kutetea taarifa ya utafiti wao".
Akizungumzia kuhusu UKAWA kupata mwaliko Wa kufanya mdahalo Wa mgombea wao Wa urais alisema kuwa hakuna taasis yoyote iliyoleta barua kwa mgombea urais,Edward Lowassa kushiriki kwenye midahalo.
"Utafiti Wa ndani Wa UKAWA uliofanywa na watafiti guru kutoka nje ya nchi ulionyesha Edward Lowassa atapata kura 74%".alisema Mbatia.
Naye Prof.Baregu alisema kuwa sampuli ya data za utafiti Wa TWAWEZA imechafuliwa kwa makusudi ili kupotosha umma.
"Mtafiti kutoka Oxford University niliongea naye aliona kuwa UKAWA inaweza kushinda ila siyo kwa gap kubwa"alisema Baregu
Post a Comment