Mkongwe na mchambuzi wa soka nchini
Ally Tembele Mayai akiwa Mkoa wa Arusha alisema kuwa Arusha kukosa hata timu
moja inayoshiriki ligi kuu ni aibu kubwa kwa wakazi na viongozi wa soka mkoani
hapa
Mayai ambaye ni mjumbe wa TFF katika
kamati ya soka la vijana, Alisema hayo, wakati wa uzinduzi wa michuano ya
airtel Rising Stars kati ya Future Stas na Chriss FC ambapo katika mchezo huo
timu hizo hazikuweza kufungana.
“wapenzi nwa soka wa Mkoa wa Arusha
wanatakiwa kuwadai viongozi wa soka wa mkoani hapa juu ya maendeleo katika
tasnia ya soka,kwa sababu miongoni mwa majiji yenye utajiri mkubwa hapa nchini
huwezi kuacha kutaja Arusha”
“Waangalie Mkoa wa Mbeya una timu mbili
Tanzania Prisons, na Mbeya City wakati Tanga unatimu tatu Mgambo, Coast Union
na Africans Sports, halafu Arusha haina ntimu hata moja yaani hii ni aibu kubwa
sana” alisema Mayai.
Aliongeza kuwa soka la Arusha liuawa na
wanaarusha wenyewe kwa kuwa maendeleo hayahitaji mtu mmoja bali ni kushirikiana
wadau wote kwa pamoja na hilo kwa Arusha linawezeka.
Akitolea mfano timu ya JKT Oljoro
inayoshiriki ligi daraja la kwanza alisema kuwa hapo ndipo wanapotakiwa kuanzia
ili kutoa aibuu hiyo katika mkoa huu.
“Sikutegemea hatasiku moja kuona wanaarusha
wanaiacha AFC ishuke hadi oligi daraja la pili kwa ilikuwa timu bora na tishio
katika eramani ya soka hapa nchini laki ajabu timu hiyo inashiriki SDL na
isipofanywa mikakati thabiti ianaweza kubaki hapo hapo” alisema Mayai
Post a Comment