Mlezi wa Jumuiya ya
wazazi wa CCM wilaya ya bahi Hebron Kipiko (Mr.Kipiko) katika picha
Mlezi wa Jumuiya ya
wazazi wa CCM wilaya ya bahi Hebron Kipiko (Mr.Kipiko) ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa
jimbo la Bahi lililopo mkoani Dodoma na
kusema kuwa anaamini anauwezo wa
kutekeleza kero na matatizo mbalimbali ya nao wakabili wananachi wa jimbo hilo.
Akizungumza na Libeneke la kaskazini blog , amesema kuwa ameona mambo mengi na matatizo
mengi yanayo wakabili wananchi wa jimbo lake na pia huu
ndio wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Bahi.
Kipiko alisema kuwa , wana
wa bahi wananafasi sasa ya kuandika historia ya
aina yake kumchagu yeye kama mgombea kwani wameona tu baadhi ya mambo ambayo
ameyafanya wakati alivyokuwa mlezi wa jumuiya ya wazazi wa ccm wilaya, pia ni mmoja wa mzazi mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na
kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa
Bahi na taifa.
“Huu ni wakati wa wananchi wa
Bahi kuandika historia ya aina yake, sit
u kwa kumchagua kwa ajili ya kuwaongoza
bali ni Mzazi mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi ya
wananchi na taifa kwa ujumla,”alisema Kipiko.
Kipiko amekuwa ni mwananchi wa kwanza kujitokeza kugombea jimbo la Bayi na ni mwana
CCM wa wa kwanza kujitokeza kuomba
ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Aidha aliainisha baadhi ya
mambo ambayo atayatekeleza iwapo atapewa ridhaa
ndani ya chama na ndani ya jimbo kuongoza ,ambapo alisema jambo la
kwanza alisema kuwa kumekuwa na tatizo la maji sana katika jimbo lake kitu
ambacho ataanza nacho pindi tu atapewa ridhaa ,atajenga Zahanati ,shule
,atatengeneza barabara pamoja na kujenga hospitali
Post a Comment