Filbert Rweyemamu
Mbunge
wa Arusha Mjini,Godbless Lema amesema uandikishaji wapigakura kwa
kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration(BVR)lililokua lianze
jana na kuahirishwa hadi Juni 16,mwaka huu katika Kata nne za jijini
Arusha limepangwa makusudi kwa lengo la kuwachosha wananchi
wasijiandike.
Lema
alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake baada ya kutembelea vituo vilivyokua vitumike kuandikisha
wapigakura na kuzungumza na wananchi waliokua wamejitokeza kuitikia wito
wa Tume ya Uchaguzi.
“Namwomba
Rais Jakaya Kikwete amwondoe Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Jaji Damian
Rubuva kwasababu ameshindwa kutekeleza majukumu ipasavyo na kuliweka
taifa katika hali ya mashaka,jambo hili ni hatari katika nchi nyingine
kuahirishwa uandikishwaji ni jambo ambalo wananchi wangekua mitaani kwa
maandamano,”alisema Lema
Awali
Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa ambaye ndiye Mratibu wa Tume ya Uchaguzi
,Richard Kwitege aliwaambia waandishi wa habari kuwa uandikishaji wa
wapigakura umeahirishwa kutokana na matatizo ya kiufundi yakiwemo kuwepo
kwa ongezeko la Kata mpya Sita na baadhi ya vifaa kutokufika kwa
wakati.
Alisema
katika mazingira hayo zoezi la uandikishaji litafanyika Juni 16,mwaka
huu baada ya kujiridhisha na vifaa kupelekwa kwenye maeneo husika huku
akitaka wananchi kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu na wazee.
Hata
hivyo,Lema alisema Chadema kimejipanga ipasavyo kupinga kila aina ya
hila ya kukwamisha wananchi wenye haki ya kujiandikisha kufanya hivyo
kwa wakati wakijua jimbo la Arusha ni ngome yao hivyo wako imara
kupingana na hali zote.
Lema
alisema inashangaza kuona kuwa suala la ongezeko la Kata kwenye Jiji la
Arusha linajulikana kwa muda mrefu na halina mantiki kwani wangeweza
kuanza uandikishaji kwenye Kata ambazo hazijagawanywa badala yake
wametoa sababu ambazo hazikubaliki.
“Hili
ni jambo ambalo halikubaliki kabisa,kwanini waanze kuandikisha kwenye
Kata zilizogawanywa kama Sombetini,Elerai na Sokon I wakati kuna Kata
ambazo Tume ya Uchaguzi ingeweza kuanza uandikishaji zikiwemo za
Daraja Mbili, Terrat na nyingine,”alisema Lema
Alishauri
Tume ya Uchaguzi kutumia weredi wa kuandikisha Jimbo moja kwa wakati
mmoja badala ya kuchagua Kata chache jambo ambalo litawavuruga wananchi.
Hata
hivyo juzi Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda katika mkutano wake na
waandishi wa habari alisema maandalizi yote yalikua yamekamilika na
kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki katika tukio hilo la
kidemokrasia
mwisho
Post a Comment