Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akihutubia wananchi waliofika
katika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid ambapo alitangaza
nia ya kugombea nafasi ya Uraisi katika uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka
huu.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Mtia nia wa Nafasi ya Uraisi ambaye ni Mbunge wa Monduli
Edward Ngoyai Lowassa amesema kuwa iwapo atapata nafasi ya kuwa Raisi wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ataiondoa nchi kwenye aibu ya kuwa omba omba
kwa mataifa ya nje licha ya utajiri wa rasilimali nyingi za madini,gesi na
mbuga za wanyama zilizopo nchini.
Lowassa amesema hayo jana wakati anatangaza nia ya kuwania
nafasi hiyo katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid vilivyoko jijini Arusha ambapo
amesema kuwa Tanzania kuendelea kuwa omba omba ni sifa mbaya kutokana na wingi
wa rasilimali.
Moja kati ya agenda zinazomsukuma kugombea Uraisi ni pamoja
na kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unaendana na ongezeko la ajira ili
kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi nchini .
“ Niliwahi kusema kuwa ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri
kulipuka hivyo inahitajika mikakati na ubunifu wa kutengeneza ajira kwa vijana
wetu ,naamini naweza katika hilo” Alisema Lowassa
Ameeleza kuwa Watanzania wengi wanahitaji mabadilko na iwapo
atapata nafasi hiyo atasaidia kuleta mabadiliko ambayo yanatarajiwa na wengi.
Akinukuu maneno ya Hayati Baba wa Taifa alisema kuwa
Watanzania wasipopata mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.
Lowassa amesema kuwa vipaumbele muhimu ni pamoja na kuwekeza
kwenye afya na elimu kutamsaidia Mtanzania kuwa na ustawi mzuri utakaoleta
maendeleo ya jamii na taifa.
Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola aliyehudhuria mkutano huo
amesema kuwa kwa hatma ya nchi yetu inahitaji kiongozi kama Lowassa ili aweze
kuifikisha nchi mahali ambapo watanzania wengi wanatamani ifike.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya
Pangani Juma Hamidu amesema kuwa safari ya matumaini kwa Watanzania imeanza
rasmi na wana matumaini makubwa na Lowassa kuwa anaweza kuiongoza nchi na
kuifikisha katika mafanikio katika Nyanja zote.
KINGUNGE URAISI NI
SUALA LA WANANCHI
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru Amesema kuwa
suala la Uraisi ni suala la Wananchi ambao ni wanaamua hatma ya Raisi
wanayemtaka na si vinginevyo .
Kingunge aliyehudhuria mkutano huo amesema kuwa wananchi
wana nafasi kubwa ya kusema Raisi wanayemtaka
na awe na vigezo gani.
“Raisi Kikwete alisema Raisi anayetakiwa awe anakubalika na
watu ndani na nje ya chama hata nyerere
alisisitiza kuwa Kiongozi lazima awe ni mtu anayekubalika na watu” Alisema
Kingunge
Amempongeza Lowassa kwa kwa kutangaza nia yake na kuanzisha
safari ya kuelekea ikulu na kuongeza kuwa Raisi wa Tanzania lazima awe na uwezo
wa kukabiliana na umasikini.
Viongozi waliohudhuria ni Pamoja na Balozi Juma Mwapachu,Mbunge
Mathayo David,Askofu Gwajima.
|
Post a Comment