PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NYALANDU AWAPA MILLIONI MIA MOJA WAFANYABIASHARA WA VINYAGO JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la vinyago jijini Arusha wakiandaa bidhaa kwa ajili ya kuuza kwa watalii wanaotembelea soko hilo maramar...
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la vinyago jijini Arusha wakiandaa bidhaa kwa ajili ya kuuza kwa watalii wanaotembelea soko hilo maramara kujipatia vinyago hivyo wanaporudi makwao kama walivyokutwa na blog hii mapema leo kabla ya waziri wa maliasili na utalii mheshimiwa Lazaro Nyalandu aliyefanya ziara ya ghafla ili kujua maendeleo yao

Waziri wa maliasili na Utalii mheshimiwa Lazaro Nyalandu kushoto akiwa na katibu mkuu wa wizara hiyo Dokta Adelhelm Meru akipewa maelezo na mwenyekiti wa soko la vinyago (hayupo pichaniI) juu ya ujenzi wa soko la vinyago maarufu kwa jina la Mount Meru curious mapema leo.  soko hilo liliungua na kusababisha hasara kubwa kwa wajasiriamali hao wapatao 250 na kutoa ajira kwa zaidi ya watu 500 

Waziri Nyalalndu na katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dk. Meru wakistaajabia ujenzi wa soko hilo la kisasa ambapo waziri huyo aliwapa msaada wa shilingi millioni mia moja kupitia shirika la hifadhi za taifa nchini TANAPA
wafanyabiashara hao wakimsikiliza kwa makini waziri wa maliasili na utalii nchini Lazaro Nyalandu alipokuwa akizungumza nao mapema leo katika soko la vinyago la mount mertu curious lililokuwa limeungua hivi karibuni

Wafanyabiashara hao wa soko la vinyago lililopo karibu na ofisi ya ccm wilaya Arusha wakishangilia mara baada ya Waziri Nyalandu alipowapa msaada wa juml;a ya shilingi milioni mia moja na kuwaahidi kuwa serikali yake na wizarara yake itahakikisha kuwa tozo ya kodi ya vinyago itafutwa ili kuhakikisha soko la vinyago linakuwa la uhakika na kutoa ajira kwa familia zaidi ya mia tano

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top