PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BARAZA LA MADIWANI ARUSHA WAJADILI UHABA WA MAJI ARUSHA KATIKA KIKAO CHA DHARURA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
   Baraza la madiwani  wa Jiji la Arusha jana wameitisha   kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili tatizo la uhaba mkubwa wa ma...


 

 Baraza la madiwani  wa Jiji la Arusha jana wameitisha   kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili tatizo la uhaba mkubwa wa maji katika jiji la Arusha.

Meya wa jiji la Arusha,  Gaudence Lyimo,akizungumza kwenye ziara ya Madiwani iliyoandaliwa na Mamlaka ya maji safi na taka Arusha(AUWSA),alisema ipo sababu ya kufanya  maamuzi ya haraka  ili kukabiliana na matatizo ya maji Arusha.
"hatuwezi kukaa kimya tukiacha hali hii iendelee lazima tukae tujadili tufanye nini kutatua tatizo hili"alisema  

Hata hivyo, Mkurugenzi AUWSA,injinia Ruth Koya alisema, tatizo la maji  kwa sasa katika jiji na Arusha linatokana na kuwepo kwa vyanzo vichache na wananchi kukata kutoa maeneo yenye maji ili yachimbwe sambamba na   uharibifu wa vyanzo vya maji.

 Koya alisema zoezi la upanuzi wa mitandao ya maji linakwama kutokana na wananchi kugomea ardhi yao licha ya kuongezeka mahitaji ya maji katika kipindi  hiki cha kiangazi.

" sasa uzalishaji wa maji umepungua hufikia  lita millioni 37,huku masika uzalishaji wa maji hufikia lita  millioni 60,kitu ambacho ni hali hatarishi kwa upatikanaji wa maji jijini hapo"alisema

Alisema kwa sasa mamlaka hiyo pamoja na kuwa na wateja 37000,wamekuwa wakipoteza maji kwa asilimia 52,huku sababu kubwa ni wizi unaofanywa na wananchi wakishirikiana na wafanyakazi wa mamalaka hiyo.

"Naomba madiwani mnilinde kwakua maisha yangu hayako salama baada ya kusimamia kwa hali na mali,kupambana na wezi wa maji,huku wezi wakubwa wakiwa ni wafanyabiashara wakubwa wa mahotel,pamoja na wafanyakazi wa mamlaka,naamini ulinzi wenu utaniweka pazuri  ,"alisema Ruth

Katika majumuhisho ya ziara hiyo baadhi ya madiwani walikiri kuwa ni changamoto hasa kwa baadhi ya watanzania kutokuwa wa kweli kunusuru tatizo hilo la maji kwa kutoa maeneo yao kwa fidia iliyowekwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza diwani wa Sombetini Ally Bananga,alisema ipo sababu ya mamlaka kusimamia huduma zao ipasavyo ikiwa ni kuboresha miundombinu yao ilikuepuka kuharibika kwa mabomba yao,ambayo ndio yanachangia kwenye upotevu wa maji.

"Miundombinu imekuwa ikiharibika kila siku,barabara zimekuwa zikiharibika kila siku huku sababu kubwa ni kuharibika kwa mambomba,badala yake unakuta barabara zinetengenezwa,kwakua bomba linavuja basi panachimba hapo kwaajili ya kutengeneza na muda haujapita linaharibika tena,kwahiyo hili tatizo haliishi tu kwenye upetevu hata uharibifu wa barabara,'alisema Diwani huyo.

Diwani wa Elerai Injia Emannuel Mpinga alitaka sheria zichukuliwe kali kwa watu wote wanaositisha zoezi hilo la upanuzi wa mitandao ya vyanzo vya maji,ikiwa ni kuchukua maeneo yao kwa kutetea maslahi ya umma.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top