Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alishuhudia kikosi cha zimamoto ambao walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.
Waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
Nao wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleza jinsi tukio lilivyotokea ambapo wananchi wamelalamikia eneo hilo kuwa limekuwa na matukio mengi ya ajali na hivyo kuomba serikali kuona umuhimu wa kuweka vituo vya zimamoto katika eneo hilo kwani magari ya zimamoto yalichukua muda mrefu kufika kwenye eneo la tukio kutokana na umbali mrefu.
Nae afisa mkaguzi msaidizi wa kikosi cha Zimamoto Hamadi Dadi ameeleza walivyopata taraari za ajali wametumia muda mrefu kufika katika eneo la tukio ingawa wametumia muda mrefu kuzima moto huo kutokana na mafuta yaliyokuwa yakivuja.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na askari walionekana muda wote kwenye eneo la tukio.
Post a Comment