Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Ili kupunguza tatizo la ajira nchini Serikali haina budi kuandaa mitaala itakayowawezesha wanafunzi kujifunza ujasiriamali na kujitegemea ili kuwasaidia Wanafunzi kuwa wabunifu na kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.
Hayo yalisemwa na Meneja wa shule za Haradali za msingi na awali Bwana Saimon Severuwa wakati wa ghafla ya kutimiza miaka kumi ya shule hiyo iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, ambapo ameishauri serikali kuanzisha mitaala hiyo kuanzia shule za msingi mpaka vyuo.
Severuwa alisema kuwa wanafunzi hao wanafundishwa elimu ya ujasiriamali ili kuweza kujiendeleza wenyewe baada ya masomo yao badala ya kusubiri ajira kutoka Serikalini sambamba na kuandaa vijana katika michezo mbalimbali ambapo mpaka sasa wanamtandao wa vijana unaoitwa jali maisha ili kuwaondoa katika maisha ya mtaani.
Pia alizungumzia suala la watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuwa katika shule hiyo wanasomesha wanafunzi 340 kwa kufadhiliwa na wahisani kutoka nje hivyo amewataka watanzania kujiunga kuwasaidia watoto hao na sio kusubiri misaada tu kutoka nje kwani kuna wakati inakosekana.
Katika kuboresha na kukuza Elimu nchini wanampango wa kujenga shule ya sekondari na mpaka sasa wameshapata kibali kutoka serikalini kutokana na maombi mengi ya wazazi wa wanafunzi wanaohitimu shuleni hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu Bwana Wilson Elisha alizindua kombe la timu ya mtandao wa jali maisha ambayo ilitarajia kucheza mechi na timu nyingine kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu Bwana Wilson Elisha alizindua kombe la timu ya mtandao wa jali maisha ambayo ilitarajia kucheza mechi na timu nyingine kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.
Pia bwana Elisha aliwasihi vijana hao kutumia ujuzi wao katika kuendesha maisha kwani wao ndiyo nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kuwa mfano hasa katika kipindi hiki cha ukosefu wa ajira.
Post a Comment