Aliyekuwa
MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni
mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania
akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam
kuhusu umuhimu wa Vijana kuwa wazalendo na kulinda amani iliyopo hapa
nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Aliyekuwa
MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni
Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania
akitoa wito kwa Watanzania kusoma na kuelewa Katiba inayopendekezwa ili
kuepuka upotoshaji unaofanywa na watu wachache kwa maslahi yao.
Frank Mvungi-Maelezo
Watanzania wametakiwa kuendeleza
amani na mashikamano uliopo kwa maslahi ya Kizazi hiki na Kizazi Kijacho kwa
kuenzi misingi ya Amani na Uzalendo iliyojengwa na Waasisi wa Taifa hili.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
salaam na aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia
ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.
Nchi ni zaidi ya itikadi na Mihemko ya watu
wachache hivyo ni lazima tuwaepuke wote
wanaotaka kuvuruga amani na utulivu uliopo
alisema Mpanju
Akifafanua Mpanju amesema hali iliyojitokeza katika moja
ya midahalo iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni ni ya kukemewa na
watu wote wanaopenda amani na wazalendo kwa kuwa vitendo hivyo vinaweza kuleta
madahara katika jamii hasa kwa makundi maalum kama walemavu,wanawake na
wataoto.
Akizungumzia Katiba inayopendekezwa
Mpanju amesema ni vyema Watanzania wakaisoma na kuilewa ili kuepuka upotoshaji
unaofanywa na baadhi ya watu kwa maslahi
yao binafsi.
Aliongeza kuwa ni vyema kuepuka kauli
zinazoweza kuleta uchochezi katika jamii hasa katika kipindi hichi ambapo baadhi ya watu wamekuwawakitumia
mwavuli wa Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanya
vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Pia Mpanju alitoa wito kwa vijana
kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu
wa amani hapa nchini kwa kuweka uzalendo mbele na kujali maslahi mapana ya
Taifa na si ya Kikundi Fulani cha watu.
Katika Hatua nyingine Mpanju alikanisha
kuhusika na vurugu zilizotokea katika moja ya midahalo hapa jijini Dar es
salaam na kudai hahusiki na tukio hilo kwa namna yoyote kama ilivyoripotiwa .
Post a Comment