PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SOKO MAARUFU LA VINYAGO JIJINI ARUSHA LAUNGUA MOTO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akitazama soko la Meru Curio Craft maarufu kama masai market lilivyoteketea kwa moto ulianza majira...

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akitazama soko la Meru Curio Craft maarufu kama masai market lilivyoteketea kwa moto ulianza majira ya jana jioni ,kushoto ni Kamanda wa Jeshi la polisi Liberatus Sabas.Picha na Ferdinand Shayo

 
Baadhi ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa kuamkia leo. 
 Wakazi wa Jiji la Arusha wakiangalia namna moto ulivoathiri soko hilo.
Bango la Soko hilo.
Hali si swari kabisa sokoni hapo.
Wengine wakiangalia kama watabahatika kuokoa chochote.
Wengine wakiokota mabaki ya mabati yaliyoungua.



Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.

Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi.

"Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo

Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top