Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya
jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga Mkutano wa kupiga vita dhidi
ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini
Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh.
Lazaro Nyalandu na wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa
Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu. Picha zote na Zainul
Mzige.
* Ataka iundwe timu kufuatilia utekelezaji wa Azimio la Arusha 2014
Na Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa
wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili
na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na
zilizo Kusini mwa Ikweta.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jioni (Jumamosi, Novemba 8, 2014) mara
baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za
kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii jijini Arusha, Waziri Mkuu alisema: “Suala hili
linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika na taasisi, wananchi na
viongozi sote kama wadau wakuu, kila mmoja anapaswa kushiriki vita hii
kama kweli tunataka tuitokomeze.”
“Kwenye
hili Azimio la Arusha na nyie waaandishi wa habari pia mna sehemu yenu
mmetajwa... wamesema wanatafuta jinsi ya kushirikiana na vyombo vya
habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma,”
alisema.
Waziri
Mkuu aliwaeleza waandishi hao kwamba Azimio hilo lina vipengele 20
ambavyo vinataka utekelezaji katika ngazi ya nchi mojamoja, ngazi na
kanda na ngazi ya kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akielekea kwenye chumba cha mapumziko kabla ya
kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na
kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto
ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu, wa pili kulia ni
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri na kulia ni
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy
Mwalimu.
“Nimepata
faraja kwamba mkutano huu haukuisha kijumlajumla tu, bali umekuja na
maazimio 20 ambayo yametengwa kwa ajili yetu sisi wa ndani, mengine
yanahusisha ushirikiano wa kikanda na yako mengine yanawahusisha wadau
wa maendeleo,” alifafanua.
Ili
kutekeleza azimio hili, nimeshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo
vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake.
Timu hii ikutane kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa
maazimio haya na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji
huo,” alisema Waziri Mkuu.
Mapema,
akizungumza na washiriki wa mkutano huo wakati wa kuufunga, Waziri Mkuu
alisema kuwepo kwa watu wa ngazi tofauti kwenye mkutano huo ni
kielelezo tosha cha umakini wao na nia thabiti ya kutokomeza ujangili
katika ukanda huu.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri mdogo wa Marekani
anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli
kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa
mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga mkutano wa
kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa
wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.
“Tumeanzisha
vita, tusisahau kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu na vita
haijaisha. Tuzidishe mapambano katika sehemu tatu: kwenye nchi
unakofanyika ujangili, nchi ambazo nyara zinapitishwa na nchi
zinazopokea ama kununua hizo nyara,” alisema Waziri Mkuu.
“Nakubaliana
nanyi kwamba hakuna nchi inayoweza kukabili suala la ujangili ikiwa
peke yake. Tunahitaji tuwe na sera mahsusi, sera ya pamoja ya
kutuunganisha na kutuongoza wakati tukitekeleza Azimio hili kwa
kusaidiana na wadau wa maendeleo,” alisema.
Alisema
Azimio hilo litaipa kazi ya ziada ya Wizara ya Maliasili na Utalii
ambapo kazi kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa wa
Azimio hilo unakuwa wa ufanisi.
Jumla
ya nchi tisa zimetia saini azimio hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan
Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Kahama, James Lembeli,
huku Waziri wa Mali asili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akifurahi jambo
ndani ya chumba cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye chumba cha
mikutano. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri mdogo wa Marekani
anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli (wa
pili kulia) kwenye chumba cha mapumziko baada ya kuwasili ukumbi hapo.
Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais
(Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika
ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye chumba maalum cha
mapumziko.
Waziri
wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akimkaribisha Waziri Mkuu
Mizengo Pinda (wa pili kushoto) kufunga rasmi mkutano wa kupiga vita
dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori
mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mh. Magese Mulongo, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais
(Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Waziri
mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi.
Catherine Novelli wakiwa meza kuu.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na wadau waliohudhuria mkutano wa
kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa
wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014 wakati akifunga rasmi mkutano
huo wa siku mbili.
Mwakilishi wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania akichukua taswira za baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea mkutanoni hapo.
Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo.
Baadhi
ya wawakilishi kutoka nchi tisa wakitia saini Azimio la Arusha la
kukabili ujangili mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni
Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda
na Malawi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwenye ufungaji wa mkutano wa
kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa
wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.
Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke, akizungumza kwa niaba ya serikali ya Ujerumani.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Mali asili na utalii,
Mh. Lazaro Nyalandu wakati wa ufungaji rasmi wa mkutano huo uliodumu
siku mbili jijini Arusha.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka ukumbini hapo mara baada ya kuufunga rasmi mkutano huo.
Post a Comment