PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAMIA YA WANANCHI WAVUTIWA NA MAONESHO YA UFUGAJI NYUKI NA MAZAO YA ASALI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Naisola Mbeeya(kushoto) ambaye ni mwanachama wa kikundi cha Naitobo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha akionesha urembo wa  asi...

Naisola Mbeeya(kushoto) ambaye ni mwanachama wa kikundi cha Naitobo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha akionesha urembo wa  asili wa jamii hiyo  na Asali.

Wanakikundi cha Ujasiriamali kutoka wilaya ya Ngorongoro,mkoa wa Arusha wakionesha asali iliyowekwa kwenye vifungashio bora.

Mjasiriamali aliyepata mafunzo kutoka taasisi ya Farm Africa,Dareda wilaya ya Babati mkoa wa Manyara.

Mwandishi Wetu,Arusha

Wafugaji wa Nyuki wilayani Ngorongoro wameiomba serikali iwasaidie kupata masoko ya uhakika ya kuuza zao la Nyuki na Asali,kwa kuwa changamoto  hiyo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu, hatua ambayoimechangia kwa wafugaji hao kutoona umuhimu wa kuzalisha zao hilo kwa wingi.

Aidha wamesema  vitendea kazi wanavyotumia wakati wa kurina asali ,kuhifadhi na kuzalisha zao la Nta ni duni ,suala ambalo wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwapatia vifaa hivyo ili kuongeza tija  katika uzalishaji na utunzaji wa mazingira.

Wakizungumza na katika  kongamano la kwanza la ufugaji nyuki barani Afrika linalofanyika jijini hapa,wamesema ipo haja kwa serikali ya Tanzania kuviwezesha vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na ufugaji nyuki .

Mkazi wa kitongoji cha Ngwaile,wilayani Ngorongoro,Abraham Molelulu amesema kuwa wamekuwa wakifuga nyuki kwa muda mrefu,baada ya kuwezeshwa mizinga 60 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA).

Amesema asali inayopatikana wamekuwa wakiitumia kubadilishana na mazao wao kwa wao kwa matumizi ya dawa na chakula kwa wakati wa kiangazi na wamekuwa wakibadilishana kwa mifugo kama ng’ombe na mbuzi na pia huitumia kwa wakati wa sherehe.

Ameongeza kuwa changamoto kubwa ni kupatikana kwa masoko,vifaa vya kuchujia na kutengeneza zao la Nta,pamoja na elimu juu ya manufaa ya Nta, aliongeza kuwa pamoja na kushiriki katika maonyesho mbalimbali lakini bado wanakabiliwa na ukosefu wa  vifaa vya kutengeneza mshumaa inayotokana na Nta.

Kwa upande wa afisa utalii wa NCAA,Edward Ngobei,amesema mamlaka hiyo imekuwa ikiendeleza utalii wa aina mbalimbali katika hifadhi hiyo,pia kuendeleza  jamii inayoishi ndani ya mamlaka hiyo ikiwemo Wamasai,Wadzabe na Wabarbaig

Amesema mamlaka hiyo imekuwa ikisimamia vikundi zaidi ya 14 vya makabila hayo kwa kuviwezesha kufanikisha shughuli za ufugaji wa nyuki kwa kuvipatia mizinga ya Nyuki,kutoa elimu ya ufugaji nyuki na kulinda mazingira.

Aliongeza kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuendeleza ufugaji nyuki na mkakati mkubwa ni kuboresha usindikaji wa Nyuki ili uwe kwenye kiwango cha kimataifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top