Na Geofrey Nyang’oro na Berdina Majinge, Mwananchi
Iringa. Polisi mkoani Iringa wanawashikilia watu watatu wakiwamo
madereva wawili wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL)
kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
alisema tukio hilo lilitokea jana saa 11 alfajiri katika kituo cha
ukaguzi cha Igumbilo mkoani hapa nabaada ya ukaguzi polisi walibaini
magunia mawili ya mirungi ndani ya gari la kusafirishia magazeti ya
kampuni hiyo.
Mungi alisema mirungi hiyo ilipakiwakatika eneo la
Chalinze mkoani Pwani na taarifa za awali zinaeleza kuwa ilikuwa
ikisafirishwa kwenda Zambia.
“Taarifa zinaonyesha kuwa gari hilo liliondoka Dar
es Salaam jana saa 5:00 usiku likiwa limepakia magazeti ya
Mwananchi,The Citizen na Mwanaspoti, yote yakiwa yanachapishwa na
Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, na ilipofika eneo la Chalinze
mkoani Pwani watuhumiwa walipakia magunia hayo ya mirungi.
“Ndani ya gunia hizo kulikuwa na mabunda 302 yenye
uzito wa kilo 121 ambayo gharama zake kwa sasa hazijajulikana kwa kuwa
bidhaa hiyo ilikuwa inakwenda kuuzwa nje na sisi hatujajua soko lake
huko likoje,”alisema.
Mungi aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ayubu
Gwabugano (33), mkazi wa Forest jijini Mbeya, Mohamed Rwamo (27), mkazi
wa Kiluvya, Dar es Salaam ambaye alikuwa anaendesha gari hilo na
mwenzake Adamu Komba (33 ),mkazi wa Mabibo, Dar es Salaam.
Kamanda Mungi alisema usafirishaji wa mirungi kupitia Mkoa wa Iringa umeongezeka kulinganisha na mwaka jana.
Alisemakuwa katika kipindi cha Januari hadi
Novemba mwaka huu jeshi hilo limekwishakamata kilo 201 za mirungi wakati
katika kipindi kama hicho mwaka jana walikamata kilo 75 pekee.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa
MCL, Francis Nanai alisema, “Jambo hili limetushtua na kutusikitisha
sana, mimi binafsi na wafanyakazi wenzangu wa MCL. Tukio hili limefanywa
na madreva wetu wakijua wazi kwamba (1) sheria ya kampuni inazuia
magari ya magazeti kubeba abiria wa aina yoyote (2) hairuhusiwi kubeba
mzigo wa aina yoyote isipokuwa magazeti ya MCL pekee. Na katika hili MCL
haihusiki kwa hali yoyote ile kwani hatujawahi, hatufanyi na hatuna
mpango wa kujihusisha katika biashara yoyote haramu.
Kwa vile kosa ni la jinai, basi sheria itachukua
mkondo wake na tunaomba vyombo vya usalama vichukue hatua kali kabisa
kwa wote waliohusika. Sisi MCL tutashirikiana na yeyote mwenye mapenzi
mema katika juhudi za kukomesha biashara haramu ya aina yoyote hapa
nchini.
Ninanchukua fursa hii kuwapa pole wasomaji wetu
kwa usumbufu walioupata kutokana na tukio hili la kufedhehesha na
ninawahakikishia kwamba jambo hili halivumiliki hapa MCL na hatua kali
za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wahusika.”
Post a Comment