PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: KIEMBA AENDA RASMI KUKIPIGA AZAM FC
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    KIUNGO mahiri wa Simba Amri Kiemba, ameanza rasmi kufanya mazoezi na klabu ya soka ya Azam Fc, ikiwa ni mpango wa kukipiga katika klab...

 

 
KIUNGO mahiri wa Simba Amri Kiemba, ameanza rasmi kufanya mazoezi na klabu ya soka ya Azam Fc, ikiwa ni mpango wa kukipiga katika klabu hiyo baada ya kukamilika kwa uhamisho wake na usajili unaoelezwa kuwa unaelekea kukamilika kwa asilimia mia.
Aidha imeelezwa kuwa Azam FC tayari ilishawasilisha barua rasmi katika klabu ya Simba SC kwa ajili ya kumuomba kiungo huyo, ambaye kwa sasa yupo kwenye matatizo na klabu yake.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Kiemba pamoja na viungo wengine wa klabu hiyo, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Haroun Chanongo walisimamishwa Simba SC kwa sababu tofauti.

Wakati Kiemba na Chanongo wakidaiwa kucheza chini ya kiwango chao tofauti na wanavyokuwa timu ya taifa, Taifa Stars- Kisiga alidaiwa kuwatolea majibu ya kifedhuli na dharau viongozi wa klabu hiyo.

Wachezaji hao walipatwa na mkasa huo baada ya timu kulazimishwa sare ya tano mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1-1 na Prisons mjini Mbeya.

Baada ya kusimamishwa kwao, Simba SC ilitoa sare tena na Mtibwa Sugar mjini Morogoro kabla ya kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting 1-0 jijini Dar es Salaam.
Wakati Kiemba aliyewahi kuchezea pia Yanga SC, Moro United, Miembeni na Kagera Sugar anakwenda Azam FC, Chanongo atapelekwa timu B na Kisiga anaweza kusamehewa baada ya kuomba radhi kwa uongozi. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top