Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) imeunda jopo la watu watano kuhakiki umri wa wachezaji
watakaoshiriki hatua ya ngazi ya Taifa ya michuano ya Copa Coca-Cola
2014.
Michuano
hiyo ya ngazi ya Taifa itafanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 13 hadi
20 mwaka huu. Uhakiki wa umri utafanyika Desemba 11 na 12 mwaka huu
wakati timu zote zinatakiwa kuwasili Shule ya Filbert Bayi mkoani Pwani
kuanzia Desemba 10 mwaka huu.
Jopo
hilo la uhakiki linaongozwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau. Wengine katika jopo hilo ni Ally
Mayay, Charles Boniface Mkwasa, Dk. Jonas Tiboroha na Richard Yomba.
Timu
16 zitakazocheza michuano hiyo inayoshirikisha watoto wenye umri chini
ya miaka 15 ni Arusha, Dodoma, Geita, Katavi, Kigoma, Kinondoni, Kusini
Pemba, Kusini Unguja, Lindi, Mbeya, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza,
Ruvuma, Simiyu na Tanga.
Vyama
vya mpira wa miguu vya mikoa vinakumbushwa kutuma TFF fomu za usajili
ambazo zinatakiwa kuambatanishwa vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji
husika.
Post a Comment