Dodoma. Hali ni tete. Ndiyo neno ambalo unaweza kulizungumza kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mji wa Dodoma tangu juzi umejaa pilikapilika zikiambatana na mikutano iliyokuwa ikijadili kashfa hiyo.
Kamati ya Uongozi wa Bunge, Kamati ya Uongozi wa
Wabunge wa CCM, Baraza la Mawaziri, kwa nyakati tofauti walikaa kujadili
ripoti ya escrow ambayo inatarajiwa kujadiliwa na Bunge Jumatano na
Alhamisi.
Leo kikao cha wabunge wa CCM kinatarajiwa
kufanyika kujadili suala hilo. Wabunge walionekana kila kona ya Viwanja
vya Bunge jana wakijadiliana katika vikundi kuhusu sakata la escrow,
huku wengine wakitaka hata miswada yote iliyobaki isijadiliwe ili kutoa
nafasi kuichambua kwa kina kashfa hiyo.
Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo.
Wabunge wa CCM wamegawanyika katika makundi
matatu; linaloshinikiza waliohusika na wizi huo wajiuzulu, kundi la watu
wasiokuwa na msimamo na kundi linalotaka ripoti isijadiliwe bungeni.
Kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika jana
asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili
badala ya moja iliyokuwa imepangwa awali.
Kamati ya Uongozi CCM
Katika kikao cha Kamati ya Uongozi wa Wabunge wa
CCM, wabunge wawili akiwemo Naibu Spika, Job Ndugai walipewa kibano
kuhusiana na matamshi yao kuhusu sakata hilo.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa
waliokumbana na kibano hicho ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na
Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya, ambao waliambiwa kwamba matamshi
yao wakati wakichangia yalilenga kukifanya chama hicho kuonekana kuwa ni
cha wezi.
“Ndugai yeye walimbana kwa nini aliruhusu mjadala huo bungeni,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.
Aidha, baadhi ya wabunge wana hofu kuwa mjadala huo huenda usiende bungeni.
“Kuna taarifa kuwa Serikali bado haitaki mjadala huu uingie
bungeni na wanamtumia Spika Anne Makinda kuukwamisha. Sisi hatuwezi
kukubali uzuiwe kujadiliwa tutapiga kura za kutokuwa na imani naye iwapo
atajaribu kufanya hivyo,” alisema mmoja wa wabunge kutoka Kanda ya
Kati.
Alisema taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa mahakama inataka kuzuia mjadala huo usiingie bungeni.
Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza
kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alitoa msimamo mkali kuhusu
sakata hilo la escrow na kwamba ametaka hatua zichukuliwe kwa wahusika
wote.
Katika kikao hicho inaelezwa kwamba Nchemba
alionyesha msimamo wake waziwazi kuwa sakata hilo ni hujuma na kwamba
haiwezekani walioiba fedha hizo wakaachiwa tu hivihivi.
Ndani ya kikao hicho imeelezwa kuwa Mwigulu
alijitokeza na kusema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) ameshamaliza utata hivyo, mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe
na wahusika wote wakamatwe.
Alisema haiwezekani watu wakawajibika tu kwa
kujiuzulu kwa kuwa huko ni kutoa tu likizo mtu akale mabilioni yake,
hivyo wachukuliwe hatua ipasavyo na kufilisiwa.
“CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa zikamatwe zote na wahusika wote wakamatwe,” alisema Mwigulu.
Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa Mwigulu
alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika
kulihujumu taifa wakamatwe na akaunti zao zikamatwe, zifilisiwe na fedha
zirudishwe kwa wananchi.
Pia aliagiza mtumishi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ambaye anatuhumiwa kuchota Sh1.6 bilioni za akaunti hiyo
afukuzwe kazi, akamatwe na akaunti zake za fedha zifilisiwe ili fedha
irudi serikalini.
Habari za uhakika kutoka kikao hicho zinaeleza
kuwa Mwigulu aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri Mkuu na
kusema kuwa kujiuzulu siyo adhabu stahiki kwa wizi mkubwa kama huo.
Mwigulu alisema: “Tazama wanafunzi, watoto wa
maskini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo, madawa hospitalini hakuna,
maskini wanakufa, watu wasio na hatia wanafungwa kwa kukosa michango ya
maabara, walimu wanadai fedha zao, wazabuni wanauziwa nyumba zao na
benki huku wakiidai Serikali kwa huduma walizotoa, leo wezi tuwape
adhabu ya kujiuzulu? Tuwape likizo ya kwenda kutumia fedha walizo waibia
maskini?”
Kwa mtumishi wa TRA aliyekula fedha za IPTL zaidi ya 1.6 bilioni Mwigulu akatoa agizo:
Post a Comment