PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAGONJWA WA KISUKARI KUPATWA UPOFU WA MACHO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  W agonjwa wa kisukari mkoani Kilimanjaro wameshauriwa kwenda kumwona mtaalamu wa magonjwa ya macho mapema kutokana na kile kilichoelezw...
 
Wagonjwa wa kisukari mkoani Kilimanjaro wameshauriwa kwenda kumwona mtaalamu wa magonjwa ya macho mapema kutokana na kile kilichoelezwa wapo hatarini kupatwa na matatizo ya macho.

Daktari wa macho na mratibu wa macho mkoani humo Dr Hilda Shangali ametoa wito huo baada ya kugundua jamii nyingi hapa nchini ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro hawana uelewa kuwa matatizo ya sukari mwilini huweza kusababisha matatizo ya upofu kwa uharaka zaidi.

Aidha Dr Shangali alibainisha matatizo hayo kuwa ni pamoja na mtoto wa jicho na uvujaji wa damu mishipa ya nyuma,hivyo kuhamua kutoa wito huo kwa jamii hususani wagonjwa wa kisukari kuwahi matibabu ya macho kabla ya kupatwa na upofu wa macho.

“Uvujaji wa damu mishipa ya nyuma ni hatari sana kwani hauna dalili zinazoonekana wala mgonjwa hapatwi na maumivu yoyote yale hivyo niwahimize tu wawahi wataalamu wa macho ili kuziba ufa kuliko kujenga ukuta”Alisema Dr Shangali.
Sanjari na hayo Hilda shangali alitoa pia wito kwa waratibu wa macho Taifa kufanya hamasa kwa wagonjwa wa kisukari kufika mapema kwa wataalamu wa macho kupata tiba na ushauri

“ Ili kwa pamoja tufanikiwe kufikisha elimu kwa jamii ya Tanzania kuwa wagonjwa wa kisukari wapo hatarini kupatwa na upofu ama matatizo mengine ya macho  niwatake waratibu wa macho Taifa nao waendeleze na kufanya hamasa kwa jamii kihusu hili”Alimalizia Shangali.

Ili pia kudhibitisha hayo gazeti la MBIU YA JAMII ilizuru baadhi ya vituo vya kutoa huduma ya afya mkoani hapo na kugundua licha ya wagonjwa hao kutokua na uelewa yakuwa wapo hatarini kupatwa na upofu pia wengi wao wameshindwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu aina ya vyakula wanavyopaswa kula kutokana na kile walichokieleza kukabiliwa na changamoto za kiuchumi pamoja na ndugu na jamaa wanaowahudumia nao pia hawaelewi umuhimu wa wagonjwa wao kutumia vyakula hivyo kila mara.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top