Kikosi cha Young Africans Sports Club
Pazia la
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara litafunguliwa leo kwa mchezo wa Ngao
ya Jamii kwa Young Africans kucheza na timu ya Azam FC kwenye dimba la
Uwanja wa Taifa kuanzia majia ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki.
Young
Africans ambayo imekua na rekodi ya kufanya vizuri katika michezo ya
Ngao ya Jamii, itashuka dimbani kupambana na wana lambalamba Azam FC
huku ikiwa na kumbumbuku ya ushindi katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu
uliopita ambapo watoto wa Jangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0,
mtikisa nyavu akiwa ni Salum Telela "Essien".
Kocha
Marcio Maximo ambaye atakua akiongoza Yanga mara ya pili katika dimba la
Uwanja wa Taifa. amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri jambo
ambalo linampa wigo mpana wa kikosi kuchagua nani amtumie katika mchezo
huo.
Mpaka
sasa Maximo ameiongoza Yanga katika michezo minne ya kirafiki
akifanikiwa kushinda michezo yote ambapo aliibuk ana ushindi 1-0
(Chipukizi FC), 2-0 (Shagani FC), 2-0 (KMKM) na 1-0 (Thika United)
kutoka nchini Kenya.
Katika
mazoezi ya mwisho yaliyofanyika leo asubuhi katika Uwanja wa shule ya
Sekondari Loyola mchezaji pekee ambaye hakuweza kufana mazoezi ni Jerson
Tegete anayesumbuliwa na nyonga, huku mbrazil Coutinho akifanya mazoezi
mepesi chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr. Suphian Juma.
Wapenzi
wa Young Africans mnaombwa kujitokeza kwa wingi kesho kuja kuwashangilia
vijana katika mchezo huo, kwani kocha mkuu mbrazil Maximo ameliandaa
jeshi lake lote kupambana na kupata ushindi kwenye mchezo.
Jumla ya
wachezaji 26 wameendelea kuwepo kambini kujiandaa na mchezo huo katika
Hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani - Kariakoo :
Wachezaji waliopo kambini ni:
Walinda mlango: Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deo Munish "Dida"
Walinzi wa Pembeni: Juma Abdul, Salum Telela, Oscar Joshua, Edward Charles na Amos Abel
Walinzi wa kati: Kelvin Yondani, Rajab Zahir, Pato Ngonyani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Omega Seme, Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu"
Washambuliaji:
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Huseesin Javu, Said Bahauzi, Andrey
Coutinho, Geilson Santana "Jaja" na Hamis Kizza "Diego"
Tayari
TFF ilishatangaza viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tshs 30,000 (VIP A)
Tshs 20,000 (VIP B & C) Tshs 10,000 (Rangi ya Chungwa) na Tshs 5,000
(Bluu & Kijani).
Ununuaji wa tiketi unafanyika kwa huduma ya M-PESA au wakala CRDB Fahari Huduma
Last Updated ( Saturday, 13 September 2014 08:18 )
Post a Comment