MAAMUZI MKUTANO MKUU CHADEMA:. MAANDAMANO NCHI NZIMA
.
Katika hali ya kawaida huwezi kuona dalili nzuri kwa nchi hii na pengine tunapoelekea ni hatari kuliko tulipotoka,mi bado nashindwa
kuelewa ikiwa makamanda wetu wanahitaji amani au hatari! ikiwa kauli hizi zinatolewa na kiongozi basi naamini ukombozi unakuja kwa kasi ambapo kama sio kumwaga damu kwa miaka 270 mfululizo basi ni kuleta mapinduzi ya shida.
hivi punde tu kulikuwa na mkutano mkuu wa chadema jijini dar es salaam, lakini kauli zilizotumiwa pale ni za kuogofya kwa wale wenye akili timamu na wale wanaotazama ushabiki basi sina shaka wamefurahia maneno hayo.
moja kati ya kauli inayonishangaza ni pale mbowe aliposema wakaazi wa dodoma waandamane wakielekea katika jengo la bunge la tanzania,na huko kunaenda kufanyika nini? mbona wao wakati wakipokea mgawo wa kwanza mwezi wa pili walifurahia na mbona hadi sasa hawaja turudishia pesa zetu sisi wananchi walizozichukua hapo awali? changa la macho hilo na bila shaka huna sababu ya kuitwa mwendawazimu ikiwa una akili nzuri ya kutafakari.
watanzania tunajisahau, tuwaangalie wenzetu, majirani zetu wanavyoteseka katika maisha yao wakati walipoikubali siasa kuinyenyekea. mfano mzuri ni somalia, DRC, rwanda,burundi, libya,misri,jamhuri ya afrika ya kati na nyinginezo nyingi, na swali unalopaswa kujiuliza mtanzania ni kwamba endapo mtaingia katika machafuko ni nani atakupokea ikiwa wote wanategemea kukimbilia tanzania?
jipange kisha tafakari kesho utalia japo leo unawaonea huruma wenzako.
Post a Comment