PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JE UNAHITAJI KUFANIKIWA?; HAYA NI MASWALI MATANO MUHIMU YAKUJIULIZA KATIKA MAISHA YAKO SEHEMU YA PILI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Habari za muda na wakati huu ndugu msomaji wa makala yangu ya kwanza kabisa kupitia blog hii, ni jambo la kumshukuru sana Mungu, kila m...




Habari za muda na wakati huu ndugu msomaji wa makala yangu ya kwanza kabisa kupitia blog hii, ni jambo la kumshukuru sana Mungu, kila msomaji ashukuru kwa imani yake.
Nitakua napata nafasi mara moja kwa kila juma kuwaandikia ninyi wasomaji wetu mambo mbalimbali yanayohusu maisha lakini yote yakilenga katika kuwafanya watu wa rika mbalimbali kujitambua na kuanza safari ya mafanikio katika yale wanayoyafanya. Tutaendelea kufahamiana kadiri siku zinavyokwenda, lakini kwa makala hii ya kwanza kabisa ningependa tuangalie kwa undani kidogo kwamba sisi ni nani, tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi.
Haya ni mambo ya msingi kabisa hasa kwa mtu ambaye yupo kwenye mchakato wa kufanikisha jambo Fulani, ni muhimu kujifanyia tathimini ili uweze kujua upo katika hatua gani katika mchakato mzima wa kufanikisha jambo lako. Kwahiyo kwa makala hii ya kwanza kabisa ningependa kila msomaji atakaepata nafasi ya kusoma makala hii ajiulize na atafakari kwa undani kabisa maswali matano ntakayoyauliza hapo chini. Lakini kabla sijaandika maswali haya napenda kuwaambia wasomaji wangu kuwa, wengi tunaamini kuwa jambo baya sana katika maisha ya mwanadamu ni kupata msiba au kufiwa kwa maneno mengine, kwa sababu inaleta uchungu sana na wengine wanafikia hatua ya kujiua kwasababu amefiwa na mtu wa muhimu sana katika maisha. Lakini mimi napenda kuwaambia kuwa jambo baya sana katika maisha ni kuishi maisha yasio na sababu. Ni mbaya zaidi kuwa hai lakini hujui kwanini, kwa sababu ukiwa hai ni lazima kutambua unafanya nini na muda wako, nguvu zako na vipaji vyako. Na ni lazima pia kujua kuwa mwaka, mwezi na siku iliopita umefanya nini juu ya maisha yako, kwa hiyo watu wengi wanaishi tu sababu wanapumua na wana nguvu za kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini hawajui kwanini wanaishi. Na ndio maana napenda kila msomaji wangu apate nafasi ya kujiuliza maswali haya matano, maswali ambayo ukiyajibu jinsi inavyotakiwa basi utaweza kujua ni kwanini mpaka leo Mungu hajakuchukua na ndio itakuwa mwanzo wako wa kuelekea safari ya mafanikio katika kile unachokifanya.
1. Wewe ni nani?, Kwanza ni swali gumu, na wengine wanafikiri jibu wanalo kwasababu mara nyingi ukimuuliza mtu wewe ni nani basi atajibu kile anachokifanya, kwa mfano Mwalimu, Dereva, Daktari, n.k. Kwahiyo hapa namaanisha wewe unajitambuaje na sio unafanya nini, usichanganye kazi unayoifanya na wewe ni nani, basi wale wasio na kazi sijui watajiitaje, kazi unayoifanya ni ya muda tu, na kama ni hvo basi ukipoteza kazi yako na pia umepoteza maisha yako. Kwahyo ni swali gumu sana la kujiuliza wewe ni nani, jipe muda na tafakari kwa undani sana juu swali hili la kwanza.
2. Wewe umetokea wapi?, Ni swali gumu sana, lakini la muhimu sana pia kujua. Na pia ni swali ambalo kwa miaka mingi sana wataalamu wa sayansi duniani kote wamekua wakijaribu kulitafutia jibu, mpaka wamefika hatua yakusema kuwa asili yetu ni sokwe, lakini hapohapo jiulize ni kwanini hawa sokwe wasasa nawabadiliki kuwa kama sisi. Kwa hiyo kumekuwa na majaribio mengi sana yakujaribu kusema tumetokea wapi, lakini napenda kuwaambia kuwa huwezi kujua wewe ni nani mpaka ujue umetokea wapi, hivyo huwezi kujibu swali la kwanza kabla hujajibu swali la pil. Hivyo ni swali muhimu sana kujua umetokea wapi na ni nini hasa chanzo chako.
3. Kwanini nipo hapa?, ni swali gumu pia, jiulize kwanini ulizaliwa?, kwanini mpaka sasa upo duniani?, kwanini umeletwa duniani?, n.k., hili ni swali gumu sana na naamini wasomaji wangu wengi mpaka sasa hawana jibu la swali hili. Kwanza kabisa ni swali ambalo wengi wetu tunajiuliza moyoni, ni mara chache sana utakuta mtu Page 2 of 4 Page 3 of 4 anaongelea jambo hili hadharani kwasababu tunaogopa kuwa hatuna majibu ya swali hili. Kwanza kabisa kilifanyika kitendo kati ya mwanaume (baba yako) na mwanamke (mama yako), mbegu za kiume zikatoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke, wanasayansi wanathibitisha kuwa zaidi ya mbegu milioni mia sita (600,000,000) zilikimbilia yai la mwanamke, na mbegu moja tu ndio ilifanikiwa kuingia ambayo ni wewe. Sasa ni kwanini mbegu zingine zaidi ya milini mia tano na tisini na tisa (599,999,999) zilikufa ili wewe uweze kuja kuishi hapa duniani?, je kuna sababu maalumu ya wewe kuzaliwa?, Kwanini mwenyezi Mungu alichagua mbegu yako wewe kuja duniani wakati huu?, Kwanini umekuja duniani ni swali gumu sana, haukuja duniani ili ulipe bili mbalimbali halafu ufe, umakuja duniani kwa kazi maalumu, umekuja kuleta tofauti na kufanya jambo ambalo litagusa maisha ya watu wengine, kwahiyo ni jukumu lako kutafuta na kujua ni jambo gani maalumu ambalo umeletwa kulifanya hapa duniani sababu hujazaliwa kimakosa. Kwahiyo kujua ni kwasababu gani umekuja duniani ni swali gumu sana.
4. Ni kitu gani naweza kufanya na ni upi uwezo wangu halisi?, hili swali gumu pia, kwasababu wasomaji wengi wa makala hii na watu wengine pia wanaishi chini ya uwezo wao halisi. Hatujui tuna uwezo kiasi gani wa kufanya mambo mbalimbali kwasababu tumeruhusu na kukubali mawazo ya watu wengine juu ya uwezo wetu, watu na jamii zilizotuzunguka zinatuambia yapi tunaweza na yapi hatuwezi kufanya. Kama wewe ni mmoja wa wahanga wa suala hili basi ni wakati wa kubadilika na kuanza kufanya mambo ambayo tunaona tuna uwezo nayo bila kujali maoni ya wanaotuzunguka. Saa zingine hata mahali tunapoishi panaweza kuwa laana kubwa juu ya mafanikio yetu kwasababu unakuta umezungukwa na watu wengi wanaokukatisha tamaa, ukiona hivyo ni wakati wa kuhama na kutafuta mahali ambapo utapata watu watakaokutia moyo katika mipango yako. Swali hapa ni kipi hasa una uwezo nacho wakukifanya, ni swali gumu kwasababu tumesharuhusu mawazo ya watu wengine juu ya uwezo wetu halisi.
5. Je ninakwenda wapi?, ni swali gumu pia, kwasababu ni swali ambalo linahusika moja kwa moja na hatima yako. Unakwenda wapi na maisha yako?, wapi utakua baada ya siku, wiki, mwezi, mwaka au miaka kadhaa?, Wapi utakua ndani ya miaka kumi ijayo?, Unaona nini baada ya miaka ishirini ya maisha yako?, Ni kitu gani unataka ufanye juu ya maisha yako kwa miaka arobaini ijayo?, Ni kitu gani unakiona ndani ya maisha yako katika hatima yako ijayo?, Ni tumaini gani linakuongoza jinsi utakavokuwa na unayotaka kuyafanya au unasubiri tu mshahara unaofuata??? Je maisha yako yanajitosheleza na bili zinazokusubiri kulipa???
Je kuna hatima yoyote ya maana unayoiona kwenye maisha yako?, Naandika makala hii kukuambia kuwa hujaja duniani kupita tu, bado upo duniani kwasababu kitu ambacho unatakiwa kukifanya bado hakijafanyika Umeumbwa kuishi maisha yenye maana na sababu, hujakosea kuja duniani, na mpaka utakapo tambua sababu za msingi za wewe kuishi hapa duniani ndipo utakaporidhika, umezaliwa kufanya jambo la muhimu sana hapa duniani ndio maana naamini kuwa sisi sote tumeumbwa kuishi kwa sababu maalumu, na tumepewa uwezo mkubwa kwa ajili ya hatima nzuri ya maisha yetu hapa duniani. Kwahyo naamini kabisa kuwa mpaka sasa watu wengi sana bado hatujaonyesha uwezo halisi tulionao kwasababu ya woga wa kujaribu na kuanza jambo jipya. Tukutane tena wiki ijayo.
Nawatakia mafanikio mema. MAONI; Anko Sam, Simu: 0715782872 – SMS/Call/Whatsup E-mail: ankosam2014@gmail.com Facebook: Samson Ndosi
CREDIT TANZANIA CLASSIC BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top