NA EMMANUEL MASSAWE
Wafanyabiashara
wa soko la kwa morombo jijin Arusha wameulalamikia uongozi wa manispaa kwa
kuwatoza kodi kubwa kulinganisha na
biashara zao
Wafanyabiashara
hao ambao ni wauzaji wa mbuzi wameulalamikia mamlaka husika kuwa wamekuwa
wakiwatoza ushuru mkubwa pamoja na kero ya kubadilishiwa uongozi mara kwa mara
Kitendo ambacho kinapelekea wafanya biashara hao kutokuwa na imani na uongozi
wa sokoni hapo
Mwandishi wa
habari Emanueli Massawe akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa mbuzi
Bwana Emanueli Kivuyo kwenye soko la kwamuorombo jijini Arusha
Picha na Jackline Malecela
Wakizungumza
na mwandishi wetu mmoja wa wauzaji wa mbuzi bwana Emmanuel Kivuyo amesema kuwa
wamekuwa wakitozwa elfu moja kwa kila mbuzi mmoja
“Apa
tumekuwa tukitozwa bei kubwa ya ushuru kwa kila mbuzi ukilinganisha bei
tunayonunulia na tunayokuja kuuzia hapa sokoni, yaani hata kama umekuja na
mbuzi mia tano hapa unaweza usiuze hata moja lakini kwa upande wa ushuru lazima
ulipe hata kama aujauza” alisema Emmanuel
Kwa upande
wa changamoto wanazo kumbana nazo ni pamoja na kushindwa kuwatambua viongozi wa
kudumu wa kutoza ushuru sokoni hapo
Bei ya mbuzi
mmoja uanzia shilingi laki moja mpaka laki moja na nusu kwa mbuzi mmoja, hivyo
inawafanya kuongeza bei hiyo hadi kufikia kiasi cha shilingi laki mbili hadi na
nusu.
“Biashara ya
mbuzi kwa sasa imekuwa ngumu sana
kutokana na ufinyu wa wateja hapa sokoni , pia kipindi ambacho mbuzi ununuliwa
kwa wingi ni siku za sikukuu” aliendelea kusema Emmanuel
Alipoulizwa
je kama kuna kero ambayo huwa wanakumbana nazo sokoni hapo wakiwa wanauza mbuzi
katika mnada,
Picha ya mbuzi wakiwa kwenye soko la kwa muorombo jijini Arusha tayari kwa mnada wa kuunzwa.
Picha na Jackline Malecela
“
tunasumbuliwa na madalali wanaokuja katika soko hilo kwa hajili ya kujipatia
wateja pili wanawasumbua sana wateja wetu wanaokujaga kuchukuwa mbuzi hapa na
pia wanawauzia bei tofauti na ya kawaida kwa kawaida mbuzi huuzwa kuanzia laki
moja mpaka laki moja na nusu lakini madalali hao upandisha mpaka laki mbili na
zaidi”,alisema Emmanuel
Na jitihada
za gazeti hili kumpata muhusika wa kitengo cha ukusanywaji wa ushuru katika
soko hilo ziligonga mwamba baada ya muhusika kukimbia alipo muona mwandishi,
pia bado tunaendelea na jitihada za kumpata mtoza ushuru huyo
Akitoa wito
kwa uongozi wa soko hilo kwa niaba ya wauzaji wa mbuzi bwana Emmanuel alitoa
kauli ya kuwaomba uongozi kusimamia swala zima la utozwaji wa ushuru pamoja na
kuakikisha wanawatoa watu wanaojiita madalali katika soko hilo pia na
kuweka sheria kali kwa yoyote atakae kiuka taratibu za soko hilo.
Post a Comment