Title: WAZIRI MKUU WA LESOTHO AMETOROKEA AFRIKA KUSINI BAADA YA JESHI KUTEKA SERIKALI YAKE
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5
Des:
...
Jeshi la Lesotho
Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane
ameiambia BBC kwamba amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya
maisha yake.Akizungumza kutoka nchini Afrika kusini,Bwana Thabane
amesema kuwa vitenmdo vya jeshi nchini humo vimesitisha huduma za
serikali na kusababisha mapinduzi. Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa maseru
zilizsema kuwa jeshi lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia
matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru. Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti. Licha ya mazungumzo ya kuleta amani
mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo
wakionya dhidi ya mbinu yoyote isio ya kikatiba. Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa masli asli pamoja na nafasi za kazi.
Post a Comment