PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAKAZI WA CHAMAZI WAGOMEA MRADI WA BARABARA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
zaidi ya  wakazi elfu 12 wa maeneo ya Chamazi na Mbande jijini Dar es Salaam, wameugomea mradi wa barabara ya njia sita iliyokuwa ipite...
Mfano wa barabara
zaidi ya  wakazi elfu 12 wa maeneo ya Chamazi na Mbande jijini Dar es Salaam, wameugomea mradi wa barabara ya njia sita iliyokuwa ipite katika eneo lao kutokana na utata uliogubikwa na uwekaji wa mipaka ya kupita barabara hiyo iliyopangwa kutoka Chamazi hadi Kisewe.
Wakazi hao wamesema kuwa mipaka hiyo imewekwa kwenye upande mmoja kinyume na utaratibu unaotaka uwekwe pande zote za mradi na kwamba hawatakubali mradi huohadi watakapofafanuliwa juu ya utekelezaji wakesambamba na ulipwaji wa fidia.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo amesema wameshangazwa na ukakasi uliojitokeza kuhusu barabara hiyo baada ya kuahidiwa kuwa ingetumia ukubwa (upana) mkubwa ambao haujawahi kujenga hapa nchini barabara hiyo itakuwa ni ya njia sita, yenye njia tatu zinakwenda na njia tatu zinarudi na kuwa mradi huo uko chini ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya watu wa China kwa kiasi kikubwa inafadhili kutengeneza barabara hiyo huku iukikadiriwa kuwa na upana wa mita 75 – 90, na itakuwa na urefu wa Kilomita zisizopungua 14 tofauti na sasa ambapo wamepima upana wa mita zaidi ya elfu moja (1,000).
“Tuliambiwa barabara itaanzia Ukonga Banana itapita pia Msongola, Chamazi mpaka Mbagala lakini hii haihusiani na upanuzi wa barabara ya Chamazi, ile inayotoka Mbagala rangi tatu kwenda kwenye uwanja wa timu ya Bakhresa, Azam FC, na awamu ya kwanza itakuwa ni ya utambuzi, kuweka alama ya eneo litakalochukuliwa na barabara, zoezi hili lingefanyika baada ya sikukuu ya Eid na awamu ya pili itafuata ambapo itakuwa ni uthamini wa nyumba na makazi wa wananchi watakaokuwemo ndani ya eneo lililotambuliwa” kilisema chanzo chetu cha habari.
Aidha, wamesema fomu ya uthamini ambayo waliahidiwa kuwa itatumika fomu No. 69 ambayo haihusishi majadiliano kati ya mnunuzi wa eneo na mwenye eneo huku utata ukitokea kuhusu ardhi ya eneo hilo ambayo inathamani kati ya shilingi 12,000 hadi 20,000 kwa (Square Meter) na kuwa maelezo hayo yalitolewa na Mthamini Mkuu wa Serikali.
Hata hivyo, wamesema “Inadaiwa kuwa huu mradi hauhusu barabara tu peke yake bali pia na ujengaji wa 'bandari kavu', inadaiwa pia huu mradi utakwenda mpaka Kisewe na kuwa sasa kuna wajanja wenye pesa kutokana na kuwepo kwa mradi huu na wao wamejipenyeza (kupitia mgongo wa wenye mradi) kuwahamisha watu ili waweze kununua maeneo kwa bei ya chini na hivyo kupata maeneo ya uwekezaji ambayo yatakuwa kando kando mwa barabara itakayojengwa”.
Awali imeripotiwa kuwa wananchi hao wanaomba wasaidiwe mawazo juu ya kitu wanachotakiwa kufanya ili wasipoteze haki zao za msingi na ukweli juu ya mradi huo huku wakilaumu usiri taarifa hiyo ambayo imekuwa ikifanywa na serikali kimya kimya bila kutangazwa hata kupitia vyombo vya habari.
Kwa upande wao Mwakilishi wa Baraza la Uhifadhi na usimamaizi wa Mazingira NEMC (hakutaka jina lake litajwe), amesema mradi huo umelenga kupunguza foleni za magari jijini Dar es Salaam na pia amewahakikishia wananchi kuwa kupitia kwa baraza hilo watamaliza tofauti zilizopo baina ya serikali na wakazi hao ili kuruhusu mradi kuendelea.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top