Katibu
mkuu wa umoja wa vijana,Sixtus Mapunda akiongea katika moja ya ziara
yake Mkoani Arusha hivi karibuni ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi kufanya
Mkoani hapa
*********
SAKATA la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha sasa kupatiwa muarubaini wake ambapo imedaiwa kuundwa timu maalumu itakayochunguza mgogoro huo.
Akizungumza
kwa njia ya simu Katibu mkuu wa umoja wa vijana,Sixtus Mapunda ameeleza
mtandao wa jamiiblog kuwa kutokana na kinachoendelea hivi sasa katika
umoja wa vijana Mkoa wa Arusha kuwa tayari Makao makuu wameshatuma timu
ya kuchunguza mgogoro huo
Alisema
kuwa tayari timu hiyo imeshawasili jijini Arusha hivyo kuanza kazi
rasmi kesho (leo)itakayopelekea kubaini ni nini hasa chanzo cha mgogoro
huo ambao unaendelea katika umoja huo wa vijana
“Taarifa
za kinachoendelea Arusha katika umoja wa vijana tayari ila tumeshatuma
timu maalumu ya kuchunguza ni nini hasa kinasababisha vurugu
hizo”Alisema Mapunda
Aidha
Mwenyekiti wa umoja huo Mkoa wa Arusha Robson Meitinyiku ameshangazwa
na utaratibu uliotumika kuwaita katika kikao cha Sekretarieti
unaotarajiwa kufanyika kesho ambapo alidai wajumbe walitumiwa mualiko
kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno(sms)
Kuhusu
kikao cha kesho (leo) kilichoitwisha na Sekretarieti ya mkoa chini ya
Katibu wake Mary Chatanda, mwenyekiti Meitinyiku alisema utaratibu
uliofanyika kuwajulisha wajumbe kuhusu kikao hicho ni wa ‘kihuni’ kwa
kuwa walitumiwa taarifa kwa ujumbe wa simu badala ya kujulishwa kwa
barua kama inavyotakiwa.
“Nashangaa
kwa kweli nimetumiwa ujumbe mfupi wa maneno na Gerald Mwadalu
tuliyemsimamisha kuwa kesho kutakuwepo na mkutano wa sekretarieti ya
Mkoa sijajua kikao hicho kitahusu nini hasa ila pamoja na hayo haizuii
mimi kutohudhuria”alisema Meitinyiku
.
Aidha alisisitiza kikao walichokifanyacha baraza la vijana mkoa na kuwatimua
Katibu wa UVCCM Mkoa Gerald Mwadalu kilikuwa sahihi licha ya kudaiwa
kuwa kilikuwa kikao feki kwa kuwa idadi ya wajumbe walikuwa wametimia
Mwadalu
akizungumza jana alisema kuwa kila kitu kitajulikana kwenye kikao cha
(leo) cha Sekretarieti ya Mkoa kwamba hawa wanapata wapi nguvu za
kufanya maamuzi ambayo ni kinyume na taratibu za umoja wa vijana.
Kwa sasa aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Katibu wa
UVCCM Mkoa wa muda Daniel Kayongo kutoka Longido
Post a Comment