Kutokana
na kuzuiliwa kwa mabasi ya ya kubeba abiria maarufu kama 'Daladala'
kufika eneo la Kivukoni, kunasababisha usumbufu kwa wakazi wa Kigamboni
wanaokuja katika ya jiji wanaposhuka kutoka katika Kivuko.
Idadi kubwa ya watu wanaoshuka kwenye Kivuko toka katika mabasi ya UDA yanayotoa huduma ya usafiri yanakuwa hayatoshelezi kuwabeba wote na kusababisha watu wengi kutembea kwa miguu kuja katikati ya Jiji.
Baadhi
ya sehemu za eneo la Soko Kuu la Samaki la Feri la jijini Dar es Salaam
zikiwa zimelundikwa takataka. Soko hili linatembelewa na wageni wengi
kwa shughuli mbalimbali.
Kuna
hatari barabara za mradi wa mabasi yaendao kasi zinazoendelea kujengwa
kugeuzwa sehemu ya kufanyia biashara. Katika picha hii, mkazi wa jijini
Dar es Salaam akiwa amepanga vitunguu katika moja ya barabara hizo
iendayo Kivukoni.
Post a Comment