Diwani wa kata ya Levolisi Ephata Nanyaro wakisemezana jambo na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka katika Uzinduzi wa jiko la shule ya msingi Levolosi iliyoko jijini Arusha lilojengwa na mhisani Daniel Materi kwa gharama ya sh milioni 25 ikiwa ni jitihada ya kuunga mkono mpango wa chakula mashuleni.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo,Arusha
Shule ya Msingi Levolosi iliyoko jijini Arusha inakabiliwa
na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunza teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo kompyuta.
Licha ya serikali kuhamasisha matumizi ya TEHAMA mashuleni
ili kusaidia kutunza kumbukumbu ya vitabu vingi na kujifunza kwa njia ya kisasa
hata sehemu zenye uhaba wa walimu bado
shule nyingi za msingi na zile za kata hazina kompyuta.
Aidha Mkuu wa shule ya msingi levolosi Elisante Kaaya
amesema kuwa wamekua wakikosa sehemu maalumu ya wanafunzi kujipatia huduma ya chakula (bwalo) na kueleza kuwa changamotonyingine
wanazokutana nazo ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishianakujifunzia
Tehama kama kompyuta.
Akisoma taarifa ya shule hiyo katika
uzinduzi wa jiko la shule hiyo lilojengwa kwa msaada wa
Mfanyabiashara Daniel Materi ikiwani njiamojawapo ya kuunga mkono juhudi
za kufanikisha mpango wa chakula mashuleni.
Elisante Kaaya amewapongeza wadau wote
waliojitoa kuwezesha watotowa shule hiyo kupata uji kwani mwakani wanatarajia
watoto watapata hudumaya chakula cha mchana shuleni hapo.
Mbunge wa Manyara Christopher Ole
Sendeka amesema kuwa ni jukumu la jamii kujitoa kusaidia watoto waweze
kusoma na kuzingatia taaluma ili waweze kufaulu.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arusha
John Mongela amesema kuwa ni juhudi nzuri zilizofanywa na ndugu Daniel
Materi na kuwataka wafanyabiashara wengine waige mfano wake.
Daniel amesema kuwa msaada huo ni
mchango wa kuisaidia jamii inayomzunguka hususani katikamasuala ya elimu ambayo
ni muhimu kwa jamii yetu |
Home
»
Matukio
»
yanayojiri ARUSHA
» HABARI PICHA-UZINDUZI WA JIKO LEVOLOSI ILI KUWEZESHA MPANGO WA CHAKULA MASHULENI
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment