Mechi ya mwisho ya Premier League leo hii ilikuwa kati ya vijana wa Jose
Mourinho Chelsea dhidi ya vijana wa Roberto Martinez Everton.
Mchezo huo wa kuvutia uliopigwa kwenye dimba la Goodson Park umeisha kwa
Chelsea kupata ushindi mzito na mkubwa kuliko wowote kwenye premier
league msimu huu.
Magoli ya mapema ya Diego Costa na Ivanovic yaliwaweka Chelsea mbele kwa
2-1 mpaka timu zilipoenda mapumziko – Kevin Mirallas aliifungia Everton
goli la kwanza dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.
Kipindi cha pili Everton walirudi kwa kasi wakijaribu kusawazisha lakini
kwenyw dakika ya 67, Coleman akajifunga na kuiongezea Chelsea uongozi,
lakini Naismith akapunguza pengo dakika 2 baadae, kabla ya Nemanja Matic
kuongeza goli la 4 kwa Chelsea.
Samuel
Eto’o akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Everton akafunga bao la 3
dk 76, lakini dakika 2 baadae Ramirez akapiga mkwaju wa 5 na Diego Costa
kwa mara nyingine tena akafunga mahesabu kwa Chelsea kwa kufunga goli
la 6 kwenye dakika 90.
Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa yakisomeka 6-3.
Post a Comment