Mtangazaji mkongwe wa michezo kwenye kituo cha redio cha Radio One Stereo, Maulid Kitenge ameacha kazi.
Katika
barua yake ya kujiuzulu, Kitenge ambaye amefanya kazi kwenye kituo
hicho kinachomilikiwa na kampuni ya IPP kwa zaidi ya muongo mmoja,
amedai kuwa anakwenda kufanya shughuli zake binafsi akidai kuwa ‘hali ya
maisha imepanda kwa kiasi kubwa sana na mahitaji ya kimaisha
yameongezeka gharama, hivyo inanilazimu kutafuta njia mbadala ya
kujiingizia kipato kikubwa zaidi.’
hata hivyo inaelezwa katika mitandao mbalimbali kuwa Maulidi kitenge amepata deal la uhakika katika kituo kipya cha radio kinachotikisa kwa sasa jijini Dar es salaam kinachokwenda kwa jina la EFM hapa chini ni picha ikimuonesha M9 akisaini mkataba mpya na mkurugenzi wa kituo hicho
Maulidi Kitenge akisaini mkataba wa kazi ili kuanza kazi rasmi na kituo cha EFM radio anayeshuhudia kushoto ni mkurugenziwa vipindi vya kituo hicho DICKSON PONELA |
Post a Comment