Sao Paulo, Brazil
WAKATI wikiendi ijayo itakuwa siku ya mwisho kwa fainali za Kombe la Dunia, kuna mambo kadhaa yametokea kwenye fainali hizo mwaka huu huku kila shabiki akiwa amejifunza.
WAKATI wikiendi ijayo itakuwa siku ya mwisho kwa fainali za Kombe la Dunia, kuna mambo kadhaa yametokea kwenye fainali hizo mwaka huu huku kila shabiki akiwa amejifunza.
Fainali hizi zimekuwa na mambo mengi ya kushangaza lakini mwishoni zinaonekana kufika kwenye hatua nzuri na ya heshima, mabingwa watetezi Hispania, timu kubwa kama Ureno, England na Italia ziliondolewa mapema sana.
Kuondoka kwa timu hizi kulifanya fainali hizo zibaki na sura nyingine ngeni kama Chile, Colombia na Costa Rica ambazo zilionyesha uwezo lakini nazo zikaishia njiani.
Leo kwenye Uwanja wa Sao Paulo, kutakuwa na mechi ngumu na ya heshima, kati ya Argentina na Uholanzi.
Mechi hii inabebwa na wachezaji wawili Lionel Messi wa Argentina na Arjen Robben wa Uholanzi.Chini kuna takwimu za wachezaji hao ambao wote watavaana kwenye mchezo wa nusu fainali leo. Takwimu hizi zinahusu fainali hizo ambazo zimeanza Juni 12 hadi leo.
Arjen Robben:
Mechi alizocheza: 5
Dakika alizocheza: 480
Mabao aliyofunga: 3
Mashuti aliyopiga: 17
Pasi zilizofika: 129
Mipira aliyopokonya: 8
Takolini: 8
Umbali aliokimbia: 55.4 km
Lionel Messi
Mechi alizocheza: 5
Dakika alizocheza: 453
Mabao aliyofunga: 4
Mashuti aliyopiga: 17
Pasi zilizofika: 180
Mipira aliyopokonya: 5
Takolini: 7
Umbali aliokimbia: 41 km
Post a Comment