Tanzania
itatia saini na Kampuni ya Mantra ili kuanza uchimbaji wa madini ya
Uranium katika eneo la Mkuju katika hifadhi ya Selous.
Waziri
wa Utalii na mali asili Lazaro Nyalandu, amesema makubaliano hayo
yatatiwa saini kabla ya mwisho mwa mwezi juni mwaka huu.
Mkataba
huo utawezesha kampuni hiyo kuanza uchimbaji wa uranium huo ukiwa ndio
mradi wa kwanza wa kuchimba masini hayo nchini Tanzania na unatarajiwa
kuiletea serikali dola milioni $640 kwa mwaka.
Waziri
Nyalandu alisema uchimbaji huo utafanyika katika eneo la kilomita 350
mraba kwenye hifadhi hiyo ilioko kusini mwa Tanzania.
Udhibiti wa shughuli za urani
Taarifa
ya serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imeahidi
kuwahakikishia Watanzania na wananchi wanaoishi karibu na maeneo
yaliyogundulika kuwepo na madini ya Urani kwa kiwango cha kuchimbwa
kibiashara, kwamba Serikali imechukua hatua kadhaa za kuweka mazingira
wezeshi kwa ajili ya shughuli za utafutaji, uchimbaji na usafirishaji
nje ya nchi madini ya Urani.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha muda mrefu Serikali kupitia Wizara
ya Nishati na Madini ilisema imejiandaa kutekeleza mradi wa madini ya
urani(uranium) katika eneo la Mkuju Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma,
huku mradi wa mto huo uliopo ndani ya pori la akiba la Wanyamapori la
Selous (Selous Game Reserve) ambayo ipo katika eneo la Sehemu ya Urithi
wa Dunia (World Heritage Site).
Kutokana
na umuhimu wa eneo hilo Mwezi Julai 2012, World Heritage Committee
iliyoko chini ya shirika la UNESCO ilitoa idhini ya kuondoa eneo la
Mradi wa Mto Mkuju kwenye eneo la Urithi wa Dunia ili uchimbaji uweze
kufanyika ambapo pia uchambuzi wa masuala ya mazingira katika eneo la
mradi wa madini ya Uranium ulikamilika mwezi Oktoba, 2012 na hati ya
Mazingira (Environmental Impact Assessment Certificate) ilitolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Post a Comment