PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mkapa atoa tahadhari kuhusu Katiba Mpya
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Aeleza umuhimu wa wananchi kuvumiliana katika mjadala hata kama watahitilafiana.   Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amewataka Watanz...


 

Aeleza umuhimu wa wananchi kuvumiliana katika mjadala hata kama watahitilafiana.   Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amewataka Watanzania kuwa waangalifu ili mchakato wa Katiba Mpya usiwe sababu ya kupigana au kufarakana ili kupata Katiba itakayoendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na ushirikiano.


Mkapa alitoa wito huo juzi, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi nyumba 30 za watumishi wa vituo vya huduma ya afya mkoani hapa zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS Foundation kwa zaidi ya Sh1.9 bilioni. “Vyovyote mchakato wa Katiba utakavyoishia, tuhakikishe tunabaki na amani na utulivu wetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu, tuhitilafiane bila kupigana,” alisema. Alisema Watanzania wanapaswa kwa pamoja wasiiharibu nchi yao na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho, vinaendelea kuwaenzi waasisi wa Taifa kwa uadilifu mkubwa. Akabidhi nyumba Akikabidhi nyumba hizo, Mkapa alisema ana imani wananchi wanaohudumiwa na zahanati 15 zilizojengewa nyumba hizo wataendelea kufaidika na huduma bora kwa kuwa watumishi wameboreshewa mazingira ya kazi. “Kama mnavyoona nyumba hizi ni za kisasa, zina maeneo muhimu yote yanayokidhi mahitaji ya binadamu, zipo imara na zimekidhi viwango vya ujenzi vinavyostahili,” alisema. Aliitaka halmashauri zinazohusika kuhakikisha nyumba hizo zinatumika kama ilivyokusudiwa, kutunzwa vizuri na kutengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya ukarabati pale utakapohitajika ili ziweze kudumu kwa muda mrefu. Vijiji vilivyonufaika vipo katika wilaya za Singida Vijijini, Iramba na Manyoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top