Wasomi, wanaharakati wahoji uhalali wa CCM kukataa rasimu ya WARIOBA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: Wasomi, wanaharakati wahoji uhalali wa CCM kukataa rasimu ya WARIOBA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema Baadhi ya wasomi na wanahakati wamehoji ni wapi Chama Cha Mapinduzi (CCM ... Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema Baadhi ya wasomi na wanahakati wamehoji ni wapi Chama Cha Mapinduzi (CCM wanapata uhalali wa kuikataa rasimu ya katiba na kuitaka itoe ushahidi kuwa mapendekezo yaliyomokwenye rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Warioba si maoni ya wananchi. Wakizungumza na NIPASHE katika mahojiano, walisema haitoshi kusema maoni si halali bila kutoa ushahidi. Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao majina yanahifahiwa kuepusha kulumbana na chama na serikali walisema hata kama ni mkakati wa chama kithibitishe madai hayo. “Wajumbe wa CCM wanaojiita kundi la wengi wanaikataa rasimu kuwa yaliyomo si maoni ya wananchi, tungependa ieleze inapata wapi uhalali wa kuyakataa? “ Wananchi walitakiwa waihoji ili ilete ushahidi siyo kuendeeleza malumbano kwa kutumia takwimu ambazo kila mjumbe anazitafsiri anavyotaka,” alisema mhadhiri mtaalamu wa taaluma za uongozi. Alisema mchakato wa katiba ya Tanzania haikufanyika kama Afrika Kusini ambayo katiba iliandikwa na Bunge Maalumu la Katiba kama lilivyo la Dodoma lenye wanasiasa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali ya kijamii. Alisema wajumbe hao baada ya bunge kuundwa kisheria walijigawanya kwenye kamati mbalimbali kama ilivyofanyika kwa bunge la Tanzania na kuunda tume ndogo miongoni mwao iliyowaendea wananchi kukusanya maoni. “Wajumbe walikusanya maoni kwenye mikutano, mtandao, simu, barua na mabaraza, baada ya kazi walirudi bungeni na ripoti ambayo bunge zima liliitumia kuandika katiba ya Afika Kusini huru,” aliongeza mmojawapo. Walifafanua kuwa wajumbe walioko Dodoma hawakukusanya maoni isipokuwa Al-Shaymaa Kwegyir , ndiye mbunge pekee aliyekuwa kwenye Tume ya Warioba, hivyo hawana uhalali wa kuikataa rasimu. “Kama wangekuwa kwenye Tume ya Warioba wangeweza kuthibitisha kuwa maoni si ya wananchi kwani wana ushahidi hawakuwepo hawana uthibitisho, wasivuruge mchakato,” alionya mhadhiri mwingine wa siasa. Alisema kwa sababu mchakato haukuwa kama wa Afrika Kusini wajumbe wasiendeleze madai aliyoyaita ya uongo kuikataa rasimu. Kwa upande wake Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, anayefuatilia mchakato huo, Harold Sungusia, alisema CCM inaposema maoni si ya wananchi inaakisi msimamo iliowahi kuutoa zamani. Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, na aliyekuwa Waziri wa Sheria, Celina Kombani, walisema Tanzania haihitaji katiba mpya. Alionya kuwa huenda chama tawala kinaendelea na fikra kuwa katiba iliyopo inahitaji kuwekewa viraka na kuendelea kutumika ndiyo sababu ya kuibua madai kama hayo. Sungusia alisema labda wajumbe hao waeleza kuwa maoni na matakwa ya CCM hayakuzingatiwa kwenye rasimu hiyo, lakini si kudai yaliyomo siyo maoni ya wananchi. Alikumbusha kuwa CCM hakikuwa na mpango wa kuandika katiba mpya na ilani yake haikuwahi kutaja suala hilo na kwamba mchakato huo umetokana na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete na siyo wa CCM. ALiongeza kuwa tangu mwanzo CCM ilikataa suala la Muungano lisijadiliwe kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya na sasa inaibuka kwa sura nyingine . Alisema kwa sababu kilichosumbua ni Muungano ushauri ulitolewa kuwa hoja irudi kwa wananchi kupitia kura ya maoni Watanzania waseme wanataka uwe wa namna gani lakini CCM ilikataa pia mapendekezo hayo. Alisema kama CCM inakataa maoni ikubali sasa kuitisha kura ya maoni ya taifa zima kujadili suala la Muungano na muundo wa serikali badala ya kuleta muundo wa serikali inayoupenda. Rasimu ya katiba imependekeza serikali tatu jambo linalipingwa na CCM na kusababisha malumbano baina yake na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao sasa wamesusia bunge hilo ambalo leo litaendelea na vikao. CHANZO: NIPASHE
Post a Comment