PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TIZAMA MCHANGO WA MR SUGU KWENYE BUNGE LA KATIBA ULIVYOSISIMUA VIJANA WA TANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wajumbe mbalimbali kwenye bunge la katiba wameendelea kuwasha vipaza sauti vyao kuchangia, kutoa ya moyoni k...


Screen Shot 2014-04-15 at 12.24.52 PM
 
2. ‘Ukarabati tu wa jengo la bunge hili ili sisi tukae zimetumika BILIONI 8.2 alafu leo kwa sababu ya hotuba moja tu ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wote wamegeuka, wanaharibu kabisa tunashindwa kufanya mambo ya maana, wanaacha kupanga mkakati wa hoja wanapanga mkakati wa kuzomea, wameishiwa mikakati mpaka wanazomea kimkakati’
3. ‘Unakutana na mbunge tena Waziri kama rafiki yangu Mwigulu Nchemba tunataniana ananiita mzee wa Maandamano mi namuita mzee wa kuteka, ananiambia wewe Sugu sijui unataka serikali tatu sijui vipi na vipi, namwambia kwani hutaki kabisa Tanganyika anasema mi nataka Tanganyika ila nataka serikali moja, sasa kama mnataka serikali moja kwa nini uibuke kwenye hoja ya serikali mbili?

5. ‘Tuko kwenye nafasi nzuri sana ya kujadili hili swala, tulijadili wakati tunaheshimiana kuliko siku tuje kulazimisha mabadiliko ambayo hatukuyapanga, tusifikie sehemu Wazanzibari hao wanaosemwa elfu sitini ndio waingie barabarani na jeshi’
 
6. ‘Mwenyekiti alikuja hapa akatutisha oooh sijui serikali tatu jeshi, Mwanajeshi atakuja atachukua nchi… Mwenyekiti mwenyewe alikua ni Mwanajeshi akavua uniform, Nyerere aliposema vueni uniform akavua na leo ni rais, kuna ubaya gani Mwanajeshi akitawala kama ana akili? hakuna ubaya, wanajeshi ni ndugu zetu’
 
7. ‘Hakuna tatizo lolote siku Mwanajeshi akija kuwa Rais kwa sababu tunae Mwanajeshi Rais Kikwete na anaendelea tu, asiweke vikwazo kwa Wanajeshi wengine ambao watakua na tija kwa taifa hili’
 
8. ‘Wanasema serikali tatu gharama, hivi kama gharama inaongezeka alafu tija inaongezeka kuna tatizo gani? ukifanya biashara rejareja ukitaka kuwa mkubwa ni lazima uongeze mtaji, kama huu mfumo wa serikali mbili umeshindwa kutuondolea matatizo mwengine anasema Znz wana hiki wana kile, mbona hamsemi kama mpaka umeme tunawalipia?? lakini sisi huku tunalia’

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top