SERIKALI YAWAPONGEZA WADAU WA SANAA ZA MAONESHO!! A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: SERIKALI YAWAPONGEZA WADAU WA SANAA ZA MAONESHO!! Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Serikali imewapongeza wahisani wa maendeleo kwa kufadhili na kukuza sanaa ambao wamekuwa wachangiaji muhimu wa kuendeleza na kukuza uchu... Serikali imewapongeza wahisani wa maendeleo kwa kufadhili na kukuza sanaa ambao wamekuwa wachangiaji muhimu wa kuendeleza na kukuza uchumi na kupunguza umasikini miongoni mwa wasanii na Taifa kwa ujumla. Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga alipokuwa akizindua programu ya “kujenga fursa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho iliyoratibiwa na asasi isiyo ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la Nafasi Arts space hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Sihaba amesema kuwa kuanzishwa kwa dhana ya Programu hii kunatoa fursa ya kujipatia kipato na kuongeza ujuzi ambao utapanua wigo wa ubunifu kwa wasanii na kuongeza mahusiano baina yao na wasanii wengine, ikiwemo kupanua soko la bidhaa zao. “Nachukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza kwa dhati Nafasi Art Space kwa uamuzi huu mahususi mlioufanya wa kuratibu uanzishwaji wa Programu ya kuibua fursa kwa wasanii wa Sanaa za Maonyesho Tanzania.” Alisema Bi. Sihaba Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sanaa imekuwa ikifanya juhudi za kutosha kuinua viwango vya sanaa nchini kwa kuanzisha programu za kitaifa na kimataifa. Aidha Bi. Sihaba alisema kuwa programu kama hizi zitasaidia kubadilishana habari, ujuzi, mikakati na ubunifu miongoni mwa wasanii kitaifa na kimataifa.
Post a Comment