PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MECKY SADICK: Jiji la Dar es Salaam tutaendelea kulisafisha!!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Jumla ya kata 22 katika manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zitaingizwa katika mpango wa utengaji wa maeneo maalum (smart area) kwa ...

Jumla ya kata 22 katika manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zitaingizwa katika mpango wa utengaji wa maeneo maalum (smart area) kwa ajili ya kuboresha usafi wa mazingira jijini Dar es salaam.

Akitoa taarifa ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa huo, Saidi Meck Sadiki, amesema uanzishaji wa maeneo maalum ya usafi wa mazingira unalenga kuondoa shughuli zote zinazofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji kinyume cha sheria na kulifanya jiji la Dar es salaam kuendelea kuwa katika hali isiyoridhisha ya usafi wa mazingira.
Amesema utekelezaji wa mpango huo unazingatia sheria ya mipango miji Na. 8 ya mwaka 2007 na sheria ya mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 na kuzitaja kata zitakazohusika katika mpango huo kuwa ni pamoja Keko, Sandali, hang’ombe, Kurasini, Mibulani na kata ya Gerezani zote za manispaa ya Temeke.
Hata hivyo amezitaja kata nyingine kuwa ni pamoja na Kisutu, Kivukoni,Upanga Mashariki, Mchafukoge, Kariakoo, Mchikichini, Jangwani, na Upanga Magharibi ambazo ziko manispaa ya Ilala na kata za Hananasif, Kinondoni, Kigogo, Mzimuni na Magomeni zote za manispaa ya Kinondoni.
Amesema kuwa ili kufanikisha  utekelezaji wa mpango huo hatua mbalimbali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuondoa shughuli zote zinazosababisha kero katika eneo husika, biashara zisizo rasmi, biashara za vyakula, uchomaji nyama na mahindi kando kando ya barabara na maeneo ya watembea kwa miguu, uondoaji wa gereji bubu, maguta, mikokoteni bajaji na bodaboda katikati ya jiji.

Shughuli nyingine zitakazofanyika ni zile za uondoaji wa malori makubwa yenye zaidi ya tani 10 katika maeneo yasiyoruhusiwa na kubainisha halmashauri zinaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli hizo.

Hata hivyo katika hatua nyingine amesema katika kuimarisha huduma za afya mkoa kupitia kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) imepitisha maombi maalum ya zaidi ya shilingi bilioni 45 nje ya bajeti ili kukabiliana na tatizo la msongamano mkubwa wa wagonjwa wa nje na wale wanaolazwa katika hospitali za mkoa wa Dar es salaam.
Aidha amesema kuwa mkoa wake unapata wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya mkoa kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini na maeneo ya karibu ambayo ni wilaya ya Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe, Mkuranga, Mafia, na wilaya ya Bagamoyo, wilaya ya Bagamoyo, Kibaha, Kibaha jambo linaloongeza mzigo kwa hospitali za mkoa huo.

Amebainisha kuwa wagonjwa wa nje sasa wanafikia 1500 hadi 2000 kwa siku jambo linalowafanya kuomba fedha zaidi kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa hospitali za rufaa za mkoa na ujenzi wa hospitali maalum kwa ajili ya mama na motto itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 600 kwa wakati mmoja.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top