PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DEREVA WA NGORONGORO CRATER ANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI KUSOMBWA NA MAJI!!!!!!!!!!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wasafiri na wanakijiji wakitizama daraja la Kirurumo lililoharibiwa kwa mafuriko na...

Mamia ya wasafiri waliokuwa wakitokea Karatu kuelekea Arusha, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, wameshindwa kuendelea na safari baada ya kushindwa kuvuka mto Kirurumo uliopo mpakani mwa Wilaya za Karatu na Monduli, baada ya mto huo kufurika na kufunika barabara kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
  Imeelezwa kuwa miongoni mwa watu waliokwama ni pamoja na watalii waliokuwa wakitoka katika hifadhi za Taifa za Serengeti na Ngorongoro, na abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la Dar Express ambalo lililazimika kurejea mjini Karatu kwa kushindwa kuvuka mto huo.
 
Abiria wengine waliokuwa wakisafiri kwa basi la Sai Baba kuelekea jijini Dar es Salaam nao hawakuweza kuendelea na safari yao kutokana na marufiko hayo.
 
Mto huo umekuwa ukiporomosha mawe makubwa kutoka milima ya Mbulu
 
Dereva wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Juma Mushi, ameponea chupu chupu kupoteza uhai katika mafuriko hayo, baada ya gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili SU 36037 kusombwa na mafuriko hayo katika mto Marera, nje kidogo ya mji wa Karatu, na kukokotwa kwa umbali wa kilometa 70 kutoka barabarani. 

Katika jitihada za kujiokoa, dereva huyo alilazimika kutoka kwenye gari lake na kupanda juu ya mti na kukaa kwa takribani saa moja mpaka pale wasamaria wema walipomuokoa na kumpeleka hospitali kucheki afya yake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top