RAIS KIKWETE AMEAHIRISHA ZIARA YAKE MKOANI TANGA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: RAIS KIKWETE AMEAHIRISHA ZIARA YAKE MKOANI TANGA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete, amelazimika kuahirisha Ziara yake huko Mkoani Tanga, kutokana na saba... RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete, amelazimika kuahirisha Ziara yake huko Mkoani Tanga, kutokana na sababu za kiutendaji. Akizungumzia kuahirishwa kwa Ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chuku Galawa, amesema Rais amelazimika kuahirisha ziara yake juzi Machi 24, mwaka huu, ambapo ataendelea nayo tena leo, ambapo amesema ujio wake umesababisha Wananchi kupata majibu ya kero zilizokuwa zinawasumbua ikiwemo kero ya upatikanaji wa Maji ya Uhakika. Aidha amesema Rais Kikwete pamoja na mambo mengine ameongea na Wananchi wa Mombo katika Mkutano wa hadhara ambapo baada ya kumaliza shughuli hiyo alilazimika kuahirisha ziara katika Mkoa huo kutokana na mambo ya utendaji wa Kazi ambapo ataenda nje ya Nchi, lakini kesho atanza tena ziara katika Wilaya ya Muheza na Wilaya ya Tanga. “Ameweza kutembelea Kata ya Makuyuni ambapo kuna maabara, inayojengwa kwa nguvu za Wananchi ambayo Rais Kikwete ameridhishwa na Ujenzi huo, na pia ameembelea Wakulima Wadogo Wadogo wa Kilimo cha Mkonge ambao wamejiunga kwenye Ushirika wao ili kujikwamua kuiuchumi” alisema Galawa. Hata hivyo amesema ujio wa Rais umewafurahisha Wananchi wa Mkoa huo, kwani miradi atakayoitembelea ataisifia na pengine kutoa maelekezo ya namna ya kuboresha utendaji kazi. Alisema alipokuwa Mombo alizungumza na Wakazi wa eneo hilo, kuhusu Kero ya maji yanayotegemewa na Wakazi hao kwa ajili ya Kilimo cha Umwagiliaji. “Pia Wananchi wa Kata ya Mombo wamemweleza hitaji lao la kutaka kupandishwa hadhi kwa Mji Mdogo, kuwa Halmashauri na suala la Afya ambapo Mheshimiwa Rais ameahidi kuyashughulikia haraka iwezeka navyo” alisema Galawa Chiku hakusema kuwa sababu ya Rais kuahirisha ziara hiyo ninini lakini Rai mwenyewe aliwaambia Wananchi kuwa amepata Dharura ya kutafutwa na Majirani zake wa karibu wanaoshirikiana nao kwa kikazi. Mkoa wa Tanga una Wilaya Nane ambazo ni Wilaya ya Handeni, Korogwe,Lushoto, Muheza, Pangani, Tanga mjini, Muheza, na Tanga ambapo kwa awamu ya Kwanza atatembelea Wilaya Nne na tayari amemaliza Wilaya mbili na kesho kutwa atamalizia ziara yake ambapo amesema zitakazokuwa zimebaki atazitembelea Mwezi Aprili mwaka huu.
Post a Comment