PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mwandishi Uingereza aibua mapya meno ya tembo Tanzania
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Mwandishi wa gazeti la Daily Mail  la Uingereza, Martin Fletcher akiwa katika chumba cha kuhifadhi meno ya tembo katika...



Mwandishi wa gazeti la Daily Mail  la Uingereza, Martin Fletcher akiwa katika chumba cha kuhifadhi meno ya tembo katika Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya meno 34,000 yamehifadhiwa. Picha ya Daily Mail. 
Dar es Salaam. Lichaya Rais Jakaya Kikwete kutoa ahadi ya kuteketeza maelfu ya meno ya tembo yaliyokwenye ghala la Serikali, imeelezwa kuwa uwezekano huo ni mdogo.Mwandishi wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Martin Fletcher ameelezakushtushwa na hali ya ulinzi kwenye ghala hilo lililosheheni meno 34,000 yatembo ambayo kwa biashara ya magendo nchini China yanagharimu Pauni 150 milioniza Kiingereza (Sh403.5 bilioni)Fletcher, ambaye aliandika habari ya kuhusika kwa wanasiasa nawafanyabiashara wakubwa wa Tanzania katika biashara haramu ya meno hayo kiasicha kuifanya nchi kuwa muuzaji mkuu wa nyara hizo, aliandika hayo kwenyetaarifa kuhusu ziara yake nchini iliyochapishwa na gazeti hilo jana.Habari ya awali ilitikisa ulimwengu ambao unapambana kulinda viumbe waliohatarini kutoweka ikiwatuhumu wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa nchinikuhusika, huku Serikali ikishindwa kuwadhibiti.Habari hiyo iliifanya Serikali ya Tanzania kufungua milango kwa vyombo vyahabari vya nje kuja nchini kupata habari sahihi kuhusu tatizo hilo, akiwamoFletcher wa Daily Mail.Katika ziara yake, Fletcher alipata nafasi ya kutembelea ghala la nyarahizo, kuzungumza na maofisa wanyama pori pamoja na Waziri wa Maliasili naUtalii, Lazaro Nyalandu.“Nyalandu pia aliweka bayana kuwa uteketezaji wa shehena ya Tanzania ni kituambacho kiko mbali na uhalisia, licha ya ahadi ya Kikwete jijini London,”Fletcher alimkariri Nyalandu kwenye habari hiyo ambayo imeambatana na pichaalizozielezea kuwa za kushtua za ghala hilo, lenye idadi kubwa ya meno ya tembokuliko maghala yote duniani.“Alisema Rais alikuwa na nia ya kuteketeza (shehena hiyo), lakini Tanzaniailitaka ilipwe takriban Pauni 30 milioni za Uingereza kutoka Jumuiya yaKimataifa kwa ajili ya Mfuko wa Hifadhi ya Tembo.”Hata hivyo mwandishi huyo anaripoti kuwa; “Wahisani ambao wangeweza kutoafedha hizo, walikejeli kiwango hicho wakisema hakina uhalisia.”Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo jana, Nyalandu alisema baadhi ya mambo kwenyehabari ya mwandishi huyo yamekuzwa, lakini alisema uamuzi wa kuteketeza nyarahizo haujafikiwa.Alisema Serikali ilichofanya hadi sasa ni kupiga marufuku biashara zote zameno ya tembo, hivyo haitauza yaliyopo na haitaomba kibali tena cha kufanyabiashara hiyo na kwamba kinachoendelea sasa ni mazungumzo ya namna yakushughulika na shehena iliyopo.“Meno mengine yaliyopo ni ya kihistoria. Ni marefu kuliko mengine na tembowa aina hii hawapo tena, hivyo kuwa nayo pia ni kitu kizuri. Haya meno ni maliya Watanzania wote, uamuzi wa kuyateketeza lazima uchukuliwe kwa busara,”alisema.Kwa mujibu wa Fletcher meno mengine yana urefu wa futi 7, uzito wa tani 125na moja linaweza kubebwa na watu kuanzia watatu, huku jino fupi likiwa na uzitowa kilo 0.4500 na kwa mujibu wa jangili aliyekiri kuua tembo 30 kwa siku, jinohilo dogo liling’olewa kutoka kwa tembo mtoto.Mara tatu katika kipindi cha miaka minane, Tanzania imeomba bila mafanikiokibali cha kuuza shehena yake kutoka katika nchi 180 zilizosaini makubaliano yakudhibiti biashara ya kimataifa ya viumbe walio hatarini kutoweka, Cites, lichaya ushahidi mkubwa kuwa kitendo cha kuuza mara moja tu, kitazidisha tamaa yaChina kupata meno hayo.Akizungumzia ziara yake nchini, mwandishi huyo anaelezea udhaifu katikaulinzi wa ghala hilo lililo nyuma ya jengo la Wizara ya Maliasili na Utaliijijini Dar es Salaam.“Ghala hilo niligundua siyo kama ngome (yenye ulinzi mkali). Lina milango yachuma ya kusukuma ikiwa na kufuli nzito tano ambazo funguo zake zimegawanywakwa maboharia wawili, lakini milango ilifunguliwa yote nilipofika,” makala hiyoinaeleza. “Kila jino limewekwa alama na namba na ghala ina kamera za ulinzi wandani, lakini sikuona mlinzi mwenye silaha nje.”Mwandishi huyo anaeleza kuwa habari yake ya kwanza iliyohoji kama mtoto waMfalme wa Wales na Waziri Mkuu wanaweza kushikana mkono na Rais Kikwete wakatialipotembelea Uingereza, ilizua kizaazaaa kiasi cha Rais Kikwete kuitisha kikaona maofisa waandamizi wa Maliasili na kutoa maelekezo kuwa wafanye kazi.Mwandishi huyo alitembelea maghala ya meno ya tembo, Hifadhi ya Selousambayo mwaka 2006 ilikuwa na tembo 70,000 lakini hadi sasa wamesalia 13,000 tu.Baadhi ya meno yalichukuliwa kutoka tembo waliokufa na mengi kukamatwa kutokakwa majangili na hayawezi kuuzwa kwa sababu ya biashara hiyo kuzuiwa duniani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top