Pichani ni wakazi wa Monduli wakisubiri kugaiwa MSAADA WA chakula na SHIRIKA LA cords |
Ugawaji wa chakula Cha mahindi ukiendelea |
NA: mwandishi wetu, Monduli
Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa Jamii( CORDS ) limetoa msaada tani 12 za mahindi ya bure kwa kaya 553 za wilaya ya Monduli mkoa Arusha, ili kukabiliana na njaa .
msaada huo umetolewa kutokana na wakazi wengi wa Monduli kukabiliwa na njaa.
Afisa Miradi wa CORDS Martha Katua amesema shirika hilo limetoa msaada huo baada ya kubaini Kaya nyingi kukabiliwa na uhaba wa chakula
Katau amesema wamegawa Tani 12 za Mahindi kwa kaya 553 katika Kata ya Mfereji Wilaya ya Monduli.
Amesema vijiji ambavyo vimenufaika na msaada huo ni Kijiji Indonyonaado ambacho kimepatiwa Tani 6.5 kwa kugawanywa kwa Kaya 301 na Kijiji cha Emuruwa jumla ya Kaya 252 zimepata Tani 5.5 za Mahindi.
Mmama akiwa anafunga Debe lake la mahindi alilogaiwa na cords |
Mwenyekiti wa Bodi ya CORDs Yohana Ordorop alisema jamii ya wafugaji Monduli inakabiliwa na njaa kutokana na ukame.
"wafugaji wanategemea kuuza mifugo ili wanunuwe chakula ila sasa ukame umeua mifugo na mingine kukonda"alisema
Kaimu Afisa Kilimo , wilaya ya Monduli Theobald Ngobya amesema wilaya hiyo inahitaji tani 28,000 za chakula.
Ngobya alisema kumekuwepo na uzalishaji mdogo wa chakula kwa misimu zaidi ya miwili mfululizo katika wilaya hiyo hatua ambayo imesababisha upungufu wa chakula.
Amesema wilaya hiyo inaupungufu wa mahindi Tani 22,550 na maharage Tani 7578 ili kupunguza tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo mengi.
Jeremiah John amewapongeza CORDS kwa kuwapa msaada wa chakula kwani wanauhaba wa chakula.
John ameomba mashirika mengine na serikali kuwasaidia.
Post a Comment