Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (katikati)
akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa
kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiwa na mgeni
wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina,
wakiingia kwenye jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya Rais huyo kuwasili nchini kwa
ziara ya kikazi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya
Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mjini Dodoma
Sehemu
ya ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ukiwa katika chumba
cha wageni Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam ukiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (hayupo pichani) aliyewasili nchini
kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho
ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika
Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza jambo wakati Rais wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto)
akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa
kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb).
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia)
akisisitiza jambo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia)
kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho
ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia
ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) na
mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) (kulia) wakigonga “tano” wakati wa mazungumzo yao wakati rais huyo
alipowasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa
mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia
anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar mjini Dodoma.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto)
na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) (kulia) wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tayari kuanza ziara ya kikazi ya
siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, DKT. AKINUMWI ADESINA, ameanza
ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli na kuahidi kuwa benki yake itawekeza zaidi ya dola za
Marekani bilioni 1 nukta 5 kwenye sekta mbalimbali katika kipindi cha
miaka miwili ijayo,
Dkt.
Adesina ameyasema hayo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na mwenyeji wake,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.
“Tunajivunia
uhusiano wetu wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza
miongoni mwa nchi za kiafrika kupata ruzuku na mikopo yenye masharti
nafuu kutoka benki yetu ambapo tangu mwaka 1971, Benki imewekeza zaidi
ya dola za Marekani bilioni 3.6” alisema Dkt. Adesina
Alisema
kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa
Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2
ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri,
miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia
Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
“Katika
miundombinu ya barabara peke yake, Benki yangu imewekeza zaidi ya dola
za Marekani bilioni 1.1 na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuboresha
usafirishaji wa bidhaa na abiria hivyo kuchochea ukuaji na uendelezaji
wa uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Adesina.
Dkt.
Adesina ameutaja mradi mwingine mkubwa wa kusafirisha umeme wenye msogo
wa kilovolti 400 wenye njia yenye urefu wa kilometa 670 katika Ukanda
wa Kusini na Kusini Magharibi mwa Tanzania, unaohusisha pia ujenzi wa
vituo vya kupozea umeme katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na
Shinyanga, wenye thamani ya dola milioni 220.
“Miradi
hii pamoja na ile wa umeme wa kutumia joto ardhi pamoja na maji
inayotarajiwa kupatiwa fedha na Benki hiyo, itasaidia sana mkakati wa
Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ambaye ammwagia sifa kwa utendaji kazi
wake mahili, wa kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika
na wenye gharama nafuu” aliongeza Dkt. Adesina.
Alisema
Tanzania imepiga hatua katika viwango vya wananchi kupata huduma ya
umeme ambapo awali ilikuwa asilimia 18 lakini hivi sasa kiwango hicho
kimepanda hadi kufikia asilimia 38 na kwamba lengo la benki hiyo ni
kutaka kiwango hicho kifikie asilimia 82 katika miaka michache ijayo.
Alisema
ili kufikia hatua hiyo Benki yake ina mpango wa kuboresha Shirika la
Ugavi wa Umeme nchini-TANESCO ili liongeze uzalishaji wa umeme wenye
gharama nafuu, kuongeza ufanisi na kutengeneza faida ili kuchochea
maendeleo ya viwanda.
Aidha,
Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, ameeleza kuwa benki
yake inasiadia kuendeleza kilimo nchini kupitia Mpango wa Kukuza Kilimo
katika Ukanda Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, kwa kukuza masoko na uongezaji
thamani ya mazao ya wakulima yanayozalishwa kupitia mradi huo.
Akizungumzia
miradi ya kikanda, Dkt. Adesina alisema kuwa benki yake imewekeza
katika miradi ya nishati ya umeme na miundombinu ya barabara ili
kuunganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Kenya ili kurahisisha
biashara na kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika nchi hizo.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameeleza
kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa
Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika nyanja
mbalimbali.
Alisema
kuwa AfDB, licha ya kusaidia kwa kiasi kikubwa kufadhili miradi ya
ujenzi wa barabara, nishati na mingine mingi na mfuko mkuu wa Serikali,
mwaja jana ilitoa pia mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 50 kwa
ajili ya kukuza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB,
zinazotumika kukopesha wakulima.
Dkt.
Mpango amesema kuwa Rais huyo akiwa hapa nchini atatembelea mradi wa
kituo cha kupooza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma na ataungana na
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua barabara ya
Dodoma-Babati hadi Arusha, iliyofadhiliwa na Benki hiyo na washirika
wake.
Post a Comment