Kambi rasmi ya upinzani bungeni imelaani na kupinga vitendo viovu
alivyotendewa Mnadhimu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu, ambaye alinusurika
kifo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, mwaka huu
mjini Dodoma
Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali moja ya Nairobi, Kenya.
Akiwasilisha bungeni maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni jana
kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/2019
kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Halima Mdee, David Silinde
alisema vitendo hivyo vinatakiwa vikemewe kwa uzito unaostahili.
Silinde ambaye ni Mbunge wa Momba (Chadema), alisema vitendo hivyo
vikiachwa viendelee bila kukemewa kuna hatari ya kundi linalohisi
kuonewa likakosa uvumulivu na hivyo kuathiri amani ya nchi.
“Ingawa miezi miwili sasa imepita tangu Lissu anusurike kifo baada ya
kushambuliwa kwa kupigwa risasi wakati mkutano wa nane wa bunge ukiwa
unaendelea na vikao vyake hapa Dodoma na mpaka sasa hakuna taarifa rasmi
iliyotolewa na serikali juu ya kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio
hilo.
“Ikiwa polisi wameshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata wahalifu hao
ndani ya miezi miwili, Kambi Rasmi ya upinzani bungeni haioni muujiza
wowote unaoeweza kutendeka ili watu hao wakamatwe na kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria hata kama polisi wataongezewa miezi mingine miwili.
“Tafsiri ya ukimya huo wa serikali ni rahisi, kwamba hakuna dhamira ya
dhati wala utayari wa kushughulikia jambo hilo. Hili la kuanza kutuwinda
kwa lengo la kutuua, hatuwezi kamwe kulinyamazia,” alisema.
Alisema Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa wito kwa wananchi wote kupaza
sauti zao kupinga uonevu na ukandamizaji wa haki, kupinga matukio ya
utekaji, utesaji na umwagaji wa damu katika nchi.
Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni
Title: Mjadala wa Tundu Lissu Waibuka Bungeni
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kambi rasmi ya upinzani bungeni imelaani na kupinga vitendo viovu alivyotendewa Mnadhimu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu, ambaye alinusurika ...
Post a Comment