Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta
Kabati akimkabidhi pesa makamu Mwenyekiti wa timu ya lipuli Ayoub nyezi
kwa ajili ya timu hiyo inayoshiriki ligi kui Tanzania bara msimu wa
mwaka 2017/2018
Kocha Mkuu wa timu ya lipuli Suleiman matola akitoa shukrani kwa mbunge huyu Ritta Kabati kwa kuichangia timu hiyo. Baadhi ya wachezaji wa timu ya lipuli wakiwa wanasikiliza kinachojili wakati walipotembelewa na mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati
Na fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati ameichangia timu ya lipuli jumla ya shilingi lakini saba kwa ajili ya matumizi ya timu ili kuisaidia timu kufanya vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara ambapo inaonekana kuwa ligi hiyo mwaka huu inaonekana kuwa ngumu.

Akizungumza
wakati wa kukabidhi pesa hizo Kabati alisema kuwa ameamua kuchangia
timu kwa kuwa anapenda michezo hivyo akiona timu ya inateteleka mara
nyingi husaidia pale kwenye uwezo wake.
"Mimi
ni muumini sana wa michezo hivyo nimekuwa nikijitolea sana kusaidia
michezo mbalimbali ndio maana umekuwa mkisikia nikifanya mambo mengi
kwenye sekta hii ya michezo,hivi karibuni nilikuwa nianzisha Mashindano
ya Ritta Kabati challenge cup ambayo imesaidia kuinua soka la mkoa wa
Iringa "alisema
Kabati
alisema kuwa ataendelea kuisaidia timu kadili awezavyo kwa kuwa
anaipenda timu ya lipuli hivyo hata akienda china ataitafutia timu ya
lipuli jezi ambazo zitawasaidia katika ligi kuu na michuano mingine
atayokuwa inaendelea hapo baadae.
Selemani
Matola ni kocha mkuu wa timu ya lipuli alimshukuru mbunge huyo kwa
msaada wake alioutoa kwa timu Utasababisha kuwapa wachezaji morali
wachezaji kuitumikia timu kwa nguvu zao zote.
"Hakuna
kitu Kizuri kama viongozi wa serikali na wanasiasa hasa wabunge
kuitembelea timu kunawafanya wachezaji kujiona wanathamani na mchango
mkuwa kwa timu na ndio mara nyingi timu kufanya vizuri" alisema matola
Kwa
upande wake kapteni wa timu ya lipuli Ally Sonso alimshukuru mbunge
huyo Ritta Kabati kwa kujitolea kuisaidia timu ya lipuli kunawapa nguvu
wachezaji kuona kuwa wanathamini na viongozi na wananchi wa mkoa wa
Iringa.
"Ukiangalia
hapa wachezaji wananyuso za kutabasamu kwa kuwa amekuja mbunge huyu
Kabati kututembelea hivyo tunashukuru sana maana hii laki mbili kwa sisi
wachezaji ni chachu kubwa sana"alisema Sonso
Naye
makamu Mwenyekiti wa timu ya lipuli Ayoub nyenzi alisema kuwa mbunge
Ritta Kabati amekuwa msaada kwa timu hii kwani ameanza toka timu ikiwa
kwenye harakati za kupanda ligi kuu Tanzania bara hivyo ni kiongozi
muhimu kwa maendeleo ya timu yetu.
"Kwa
kweli hadi saizi hakuna viongozi waliotoa kiasi kikubwa cha Pesa kama
mbunge huyu Kabati tunashukuru sana kwa mchango wake ambao unatija kubwa
sana kwenye timu" alisema Nyenzi
Post a Comment