UMOJA
wa Mataifa umepongeza mashirika mbalimbali na serikali ya Tanzania kwa
kuchukua hatua kukabiliana na vitendo vya kikatili vya ukeketaji.
Aidha
imepongeza wito kutoka katika mashirika mbalimbali ya kutaka kuwapo na
mabadiliko katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuzuia ndoa za
utotoni.
Katika
taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam
imesema kwamba kitendo cha kuwapo na ushawishi wa kutaka mabadiliko kwa
sheria hiyo ya ndoa ni dalili kwamba watanzania wanataka kuona kwamba
ndoa za utotoni zinamalizwa.
Msemaji
wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu amesema katika taarifa hiyo kwamba
kitendo cha saini kuendelea kuchukuliwa wakati wa siku ya kimataifa ya
kupiga vita ukeketaji Februari 6 mwaka huu kunaonesha kwamba watanzania
wako tayari kuzuia ndoa za utotoni.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2010, asilimia 15 ya watanzania
wamekeketwa, huku wengi wakiwa mkoa wa Manyara asilimia 77.
Kwa
mujibu wa Azimio la Beijing dunia ilikubaliana kwamba mtoto wa kike
asilazimishwe kuolewa na pia umri wa kuolewa unapaswa kuwa miaka 18.
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtoto wa miaka 15 anaweza kuolewa huku akiwa na miaka 14 mahakama inaweza kuridhia ndoa.
Taarifa
ya Umoja huo imesema kwamba Tanzania pamoja na nchi nyingine ubaguzi
kwa mwanamke unaendelea kupitia sheria na tamaduni mbalimbali huku imani
za kidini zikiimarisha ubaguzi huo.
Umoja
wa Mataifa umesema kwamba unajisikia fahari kufanyakazi na serikali ya
Tanzania kutekeleza makubaliano ya kimataifa kubadili umri wa kuozwa na
kuoa kwa vijana wake.
“Umoja
wa Mataifa unafurahi kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha
kwamba haki za wasichana zinalindwa. Pia juhudi za jamii kumaliza
ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zinakaribishwa. “ilisema taarifa
hiyo.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi ambazo mwaka 2015 zilitia saini utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu yenye lengo la kuwezesha mabadiliko
kubadili yanayostahiki karne ya 21.
Malengo hayo yamelenga kukabili changamoto za umaskini,usawa na ukatili dhidi ya wanawake.
Katika malengo hayo uwezeshaji wa wanawake ni sharti mojawapo na imeelezwa wazi katika lengo namba tano la usawa na uwezeshaji.
Lengo hilo limedhamiria kuondokana na tabia mbaya kama za ndoa za lazima na ukeketaji.
Post a Comment