Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla (aliyekaa) akiwa katika ibada maalum ya kuombea wagonjwa duniani iliyofanyika leo katika Hospitali ya Ndala,Nzega Mkoani Tabora. Wengine kulia ni Rudrovic Mwananzila na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jacqueline Liana.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi
Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli
kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya,
bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Aidha
Dkt. Kigwangalla alisema watafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na
taratibu ili kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu ipasavyo.
Dk.Kigwangalla
ameyasema hayo leo 11 Februari wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada
maalum ya kuwaombea wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika
jimbo kuu la Tabora na baadae kwenye Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya
Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.
“Tutaendelea
kutumbua majibu bila ya kmwonea mtu kwa kuwa tunafanya hivyo kwa
kuangalia sheria, kanuni na taratibu. Haiwezekani mtu akaiba dawa ambazo
zinawasaidia wananchi masikini, halafu sisi tukamwaangalia tu,” alisema
Dkt.Kigwangalla.
Alisema majipu hayo yatatumbuliwa kwa watendaji ambao watakaozembea, wasio waadilifu na wasiowajibika katika sekta hiyo ya afya.
Aliongeza
kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa inafanya kazi kwa kuwafuata
wananchi hususani wanyonge (masikini) mahali walipo ili kuhakikisha
baada ya miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa na maendeleo ya kiwango cha
juu.
Naibu Waziri huyo aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea kwa kuwa kazi ya kutumbua majibu si rahisi.
Aliuomba
uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato kwa
kutumia njia ya ki-elekroniki kwa sababu umeonyesha matokeo chanya
katika hospitali nyinigine.
Akizungumzia
kuhusu suala la upungufu wa bajeti, Dkt. Kigwangalla alisema ni vema
viongozi hao wadini, asasi za kijamii na taasisi zisizo za kiserikali
zinazotoa huduma za afya kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza fedha za
kuboresha huduma hizo, kwa kuwa si sekta hiyo pekee yenye changamoto
hiyo.
Pia vipaumbele vya shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi viko vingi, wakati rasimali fedha haitoshelezi.
Aliwataka
uongozi wa hospitali hiyo na nyinginezo za mashirika ya hiari
kuwasilisha taarifa za (data cleaning) UTUMISHI ikiwa ni pamoja na
kuorodhesha watumishi wanaotakiwa kuondolewa kwenye malipo ya mshahara
ili waweze kupatiwa kibali cha kuajiri kwani bila kufanya hivyo kibali
hakitaweza kutolewa.
Dkt.
Kigwangalla aliongeza kwamba hivi sasa wizara yake iko katika mchakato
wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za matibabu za kwa
kutumia mifuko ya bima ya afya.
Maadhimisho
hayo ni ya kila mwaka ya siku 11 Februari, Wakristo wote wanafanya sala
maalum ya kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na maradhi na kuwaombea
wapone haraka huku wakiyapokea mateso hayo na kuyaunganisha na mateso ya
kristo na kanisa lake hii ni pamoja na kuwaombea ndugu wa wagonjwa
katika kuwasaidia wagonjwa wao wakati wa kuwauguza.
Maadhimisho hayo yanaenda sambamba pamoja na kuwahudumia na kutoa misasada mbalimbali.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludocivk Mwananzila aliwataka
Watanzania kuwa na tabia ya kuwatembelea wagonjwa na wafungwa ili waweze
kupata faraja.
Kihistoria,
Hospitali hiyo ya Ndala, ilianza miaka ya 1930 kama Zahanati ndogo
chini ya Masista Wamissionary wa Afrika (Missionary of Our Lady of
Afrika-White Sisters) katika jimbo kuu hilo la Tabora
Mwaka
1963 ilikuja kuwa Hospitali kamili huku ikianza na vitanda 115 na
wauguzi 15 na daktari mmoja, hata hivyo hadi sasa ina jumla ya vitanda
152, wafanyakaz 125 huku wakiweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje
wapatao 38,917 na wagonjwa wa kulazwa 8,428.
Hospitali hiyo baadae ikapandishwa ngazi ya Hospitali huku ikiwa na vitanda 152 huku ikiwa na madaktari mbalimbali.
Wakitoa
shukrani zao ni pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya
kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya
watumishi, posho za watumishi, vitanda vulivyohainishwa, madawa,
mafunzo ya watumishi, na mambo mbalimbali.
Post a Comment